Umri Wa Mtoto Kutambaa

umri wa mtoto kutambaa

Watoto wanaanza kutambaa wakiwa na miezi 6-10 na kutembea wakiwa na miezi 8 -18, watoto huwa wanatofautiana kwenye stage za ukuaji wengine wanawahi wengine wanachelewa. Wazazi wengi wanakuwa wanasubiri kwa shauku  kubwa  Kuona watoto wanapoanza kutambaa bila  kujua  hatari zake ,iwapo mama hatokuwa makini kwa mazingira ya nyumba  Yake!

 

Unatakiwa kuzingatia haya.

 • Nyaya za umeme -zinazo ning’inia au achwa wazi -zifungwe vizuri ,
 • chaji za simu-watu wengi wamezoea kuacha Kwenye umeme ni hatari iwapo akaiweka mdomoni basi inaweza msababishia kurushwa na umeme na kumsababishia kifo, hakikisha unachomoa chaji baada ya kutumia.
 •  Pasi ya umeme au mkaa iwekwe mbali baada ya matumizi.
 • Vitu vya hatari kama kisu,mikasi,uma kwenye mnakabati la vyombo toa hivyo vitu kwenye madroo sababu ndio sehemu wanayopenda zaidi.
 • Madawa ,mafuta ya taa vyote viwekwe mbali ili asile.
 • Jikoni-hakikisha unapopika chakula  asiende kucheze jiko na kuangukiwa na jiko la mkaa au chakula cha moto kikamuunguza vibaya na kumsababishia kifo.
 • Vinywaji  vya moto au chakula  !hakikisha unaweka mbali na mtoto.
 • Maji moto-unapotaka mwogesha mtoto hakikisha hujamwacha na Maji moto ,changanya Maji kabla ujampeleka sehemu ya kuoga ,ukimwacha na Maji moto ukafata ya baridi ili uyachanganye ,ukirudi utamkuta kesha weka mikono na kungua!
 • Hakikisha sehemu unazomweka mtoto kucheza ni safi na salama -hakuna uchafu au pesa kama coins,misumari,vifungo,pini, vipande cha chupa n.k ni hatari anaweza kuvimeza, mtoto anahitaji nafasi isiyo na msongamano wa vitu ili awe huru kucheza.
 • Kitanda-mtoto  akilazwa kwenye kitanda cha wazazi  hakikisha mnamchungulia mara kwa mara ,pindi amkapo asianguke chini sababu kitanda hakina usalama kama kindanda cha watoto chenye kingo.
 •  Dressing table– hakikisha mtoto hafiki  hapo na kula perfume na urembo mwingine.
 • Mda wa kula- weka chakula mbali na yeye ni rahisi kukimwaga!
 • Chooni-ni sehemu wanayopenda watoto kuchezea haswa kwa wale wenye vyoo vya ndani muwe makini ni rahisi kubeba bakteria au virus.