
Mama anapofikisha miezi mitatu ya mwisho wiki 37-40(third trimester) anaanza kuwaza dalili za uchungu zipoje ,atazijuaje n.k .Dalili za kwenda labor zipo nyingi na kila mama zinamjia kiutofauti ,kuna umuhimu wa mama kuzijua.Uchungu huwa unakuja kwa masaa na kila muda unavyozidi kwenda ndipo dalili hubadilika. Kuna dalili za awali (pre -Labour ) na za mwisho.
Dalili za uchungu kwa mama mjamzito (labour sign)
Kabla mama hajajifungua huwa anapata dalili za awali kuashiria muda wa kujifungua unawadia, dalili inaweza kumudu kwa wiki au masaa ,dalili hizo ni
:Maumivu ya mgongo -mishipa na viungo vya mama vinajiandaa kumtoa mtoto ndipo ,kumsababishia maumivu ya mgongo.
:Maumivu ya tumbo chini ya kitovu (mtoto anapojisogeza kuja chini)
:Kuhara (diarrhea)-mishipa ya mama inakuwa ishalegea kwa ajili ya kumtoa mtoto ,inamsababishia kuhara .
:Kuvuta ukeni (contrations) ,uke utahisi unavuftwa mara 3-5 kila baada ya dakika 10 ,maumivu yanakuja kukimbia
:Kutokwa maji kwa wingi ukeni unaosababishwa na (kupasuka kwa chupa)
:Kuchoka sana , kushindwa kulala na kuishiwa nguvu.
:Kutokwa na maji maji (discharge) yenye rangi brown au nyekunde.
DALILI HIZI NI HATARISHI UKIZIONA ,WAHI KITUO CHA AFYA.
:Chupa ya maji ikipasuka ukaona rangi ya kijani au brown ni hatari ,inaweza ikawa mtoto kajisaidia inaitwa iyo hali huitwa ”Meconium” ,huwa inatokea kwa wale wamama waliopitiliza siku zao kujifungua.
:Ukisikia kizunguzungu,maumivu ya kichwa na kuvimba kwa mikono au miguu wahi hospital iyo ni dalili ya kifafa cha uzazi.
:Chupa ya maji ikipasuka kabla ya uchungu au dalili yoyote ya kujifungua usikae nyumbani zaidi ya masaa 5-6, mtoto atakuwa kwenye hatari ya kupata infection kupitia njia ya uzazi au kitovu kuhamishwa toka sehemu husika na kushindwa kumpelekea mtoto hewa ,ikamsababishia kifo au matatizo ya ubongo wahi kituo cha afya.
NB: Unapohisi hizo dalili za uchungu vizuri kuwa na simu karibu yako, ili utoe taarifa kwa ndugu au jamaa ili upate msaada mapema.