Usafi Wa Chupa Za Watoto :Jinsi Ya Kuzisafisha

Matumizi ya chupa za chuchu za mpira (bottle feeding) kwa matumizi ya watoto ni nzuri  zinarahisisha mtoto kunywa kwa urahisi ila ni hatari kwa afya ya mtoto,iwapo mzazi hatozingatia usafi basi mtoto anahatari ya kupata maradhi kama kuhara,infection au maumivu makali ya tumbo.

image

Chupa kawaida inatabia ya kutengeneza uterezi kwa ndani  ikiwa haisafishwi kwa brush lake kwa  kusugua  ndani,uterezi huo unakuja kuzalisha bacteria watakao mshambulia mtoto akiwa anakunywa maji,juice au maziwa n.k

image

Chupa za plastic zinazo tengenezwa kwa kutumia material ya bisphenol sio nzuri  kwa afya ya mtoto baada ya kufanyiwa tafiti mwaka 2012 wakashauri zisitumike na nivizuri mzazi akasoma maelezo ya chupa kabla ajanunua. Chupa zenye material ya glass ni nzuri zaidi kwa matumizi ya mtoto hata kupashia maziwa haina tatizo kama ya plastic ni rahisi kuyeyuka na sumu kuingia kwenye maziwa.

image
HIZI NI CHUPA ZA TOMMEE TIPPEE ZINASIFIKA KWA UBORA KAMA ZA AVANT ZOTE NI NZURI JAPO NI GHARAMA ZA JUU

Vituo vingi vya afya hawashauri wazazi kutumia chupa za watoto sababu wengi wanashindwa kuzisafisha vizuri na kupelekea watoto kupata maradhi.Kuna aina nyingi za chupa ila mimi ninapendelea chupa za Avant zina ubora mzuri kwa materials wanazotumia na wanachombo special cha kusafishia chupa zao(steam sterilizer)

 

Mtoto afunzwe kutumia kikombe mapema akiwa na miezi 6 itamsaidia zaidi na kujiepusha na maradhi

 

Jinsi ya kusafisha chupa ya mtoto

Tumia brush la kuoshe chupa ambalo utasugulia mule ndani kutoa uterezi  ,chuchu ibidue geuza ndani nje nje ndani nayo usafishe utaosha kwa maji safi baada ya hapo fungua chupa kwa tenganisha mifuniko,chupa, chuchu na ile ring yake ya kukazia chupa wakati wa  kufunga .

 

image
BRUSH ZA KUOSHEA CHUPA IZO NDEFU NI ZA CHUPA,IZO FUPI NDOGO NI ZA CHUCHU KULE MBELE NDANI MTOTO ANAPO NYONYEA

Bandika sufuria jikoni weka maji ya kutosha dumbukiza chupa na uache zichemkie kwa dakika 5-10 ili kuuwa vijidudu ,baada ya hizo dakika epua mwaga maji baada ya kuosha chukua kitambaa safi cha vyombo  ,tandika sehemu safi na kavu mfano kwenye meza weka chupa zake geuza juu chini ili maji yatoke na zibaki imekauka.

 

image

 

 

Kuna kifaa kinaitwa Steam sterilizer cha kuchemshia chupa za watoto nazo ni zuri zinasafisha vizuri na kuuwa bacteria

 

image

Ushauri wa afyaborakwamtoto

 

Mama hakikisha hili zoezi unalifanya mwenyewe  kuosha chupa kiufasa kabsa, kama unamwachia dada wa nyumbani kusafisha hakikisha umemfunza vizuri .Nunua chupa ziwe zaidia ya 3 itamsaidia mtoto kubadili kwa urahisi tofauti na akiwa na moja hiyo hiyo ni ngumu kuoshwa kwa kila mara baada ya kutumika na nunua chupa za glass iwapo ukapo nunua ya plastic usinunue yenye (bisphenol A) iyo ni sumu mbaya kwa mtoto.