Upungufu Wa Maji Mwilini Kwa Mtoto Mchanga(Infant Dehydration)

Upungufu wa  maji mwilini kwa watoto wachanga unaweza kutokea wakati wowote.Upungufu wa maji unaweza kusababishwa na mambo mbalimbali kama vile;  joto kali , mtoto kutonyonyeshwa baada ya muda mrefu  saa 2-4, matatizo ya kiafya pia huchangia mtoto kupoteza maji mwilini kama kutapika ,kuharisha au homa kali.

Kuna hatari kubwa kwa mtoto iwapo atapungukiwa maji mwilini .Mzazi atatambua vipi iwapo mtoto ana upungufu wa maji mwilini.

DALILI YA UPUNGUFU WA MAJI KWA MTOTO

– Mtoto kukojoa  mara chache sana, anaweza kuchukua saa 4-6.

– Nepi au diaper kuchukua muda kujaa na kuwa rangi ya njano na yenye harufu kali.

– Ngozi ukiivuta inachukua muda kurudi juu au katika hali yake ya awali.

 

– Mdomo ( lips) kuwa kavu sana mpaka kupasuka pasuka

– Machozi hayatoki  akilia

– Kuishiwa nguvu na kupata tabu kupumua

– Kukosa hamu ya kula

– Macho kulegea sana na kuingi ndani

– Ngozi  kusinyaa kama ya mzee.

– Kwa mtoto mchanga  utosi wake unabonyea  ndani.

 

 

Matatizo mengi  ya kiafya yanaweza kujitokeza iwapo mtoto akipungukiwa na maji  mwilini.  Mathalan  kupanda kwa joto kwa kiasi kikubwa hivyo kuathiri  ubongo na viungo (organs) vingine mwilini.  Vilevile kusababisha kifo  au matatizo mengine mengi  kiafya.

  TIBA

Wahi kituo cha afya kwa msaada zaidi iwapo utaona dalili  hizo zilizotajwa hapo juu.

Kwa mtoto mchanga ,mama unatakiwa kumnyonyesha   kila baada ya dakika 30-60 na iwapo mnaishi kwenye mazingira yenye joto kali , unaweza kumpa maji kidogo kijiko cha chai 2-3.

Watoto wenye umri zaidi ya mwaka 1 wanatakiwa kunywa maji kwa wingi zaidi na unaweza  kumtengenezea mchanganyiko wa maji ,chumvi na sukari akanywa. Usimvalishe nguo nyingi au nguo nzito kwenye mazingira ya joto.