Upungufu Wa Amniotic Fluid,Chanzo Chake,Madhara Na Matibabu Yake.

Aminiotic fluid  ni maji yanayopatikana tumboni mwa  mama mjamzito ,yanamzunguka mtoto kwenye hatua zake zote za ukuaji.Amniotic fluid ni muhimu sana kwa sababu yanasimamia ukuaji wa mtoto haswa kwenye misuli(muscles) miguu,mikono,mapafu na mfumo wa kusaga chakula (digestive system).

 

picha ikionyesha mtoto akiwa ndani ya amniotic fluid na kwa nje akifunikwa na amniotic sac

 

Mtoto anapoanza kupumua na kujigeuza kipindi cha

(second trimester) huwa  anasaidiwa na amniotic fluid. Kitendo hicho kinamfanya  mtoto kunywa amniotic fluid na kuja kuitoa mwilini kama mkojo. Kupungua kwa amniotic fluid kitaalamu kunaitwa oligohydramnios. Kuna sababu tofauti zinazomsababishia  mama kupungukiwa na kiasi cha amniotic fluid . Mama mjamzito anapopimwa kiwango cha amniotic fluid na ikaonyesha ni chini ya sentimita 5 , hapo inamaanisha  ni chini ya kiwango.

 

AMNIOTIC FLUID

Ina kazi nyingi tofauti kwa mfano:

 • Inasaidia kumlinda mtoto iwapo mama atajigonga au kuumiza tumbo.
 • Inasaidia kwenye ukuaji wa mfumo wa mmeng’enyo wa chakula (digestive system) na mfumo wa upumuaji wa mapafu.
 • Inamkinga mtoto na maradhi yanayo ambukiza  (infection).
 • Inamtengenezea mtoto joto mwilini.

SABABU ZINAZOSABABISHA KUPUNGUA KWA AMNIOTIC ACID

 • Matatizo ya placenta iwapo haitakuwa na kiasi cha damu ya kutosha, au kutopitisha virutubisho vya kutosha kwenda kwa mtoto, hapo ndipo husababisha kupungua kwa amniotic fluid.
 • Kuharibika kwa membrane.
 • Mama anapopitiliza siku zake za kuzaa mpaka wiki ya 42 , hapo anakuwa na hatari kubwa ya kuishiwa amniotic fluid.
 • Madhara anayoyapata mama kipindi cha mimba, mfano; kuishiwa na maji mwilini (dehyration), kisukari(diabetes), mapigo ya moyo kwenda juu (blood pressure), kifafa cha uzazi n.k  ndio huchochea kupungua kwa amniotic acid.
 • Matumizi ya madawa makali kipindi cha ujauzito( ibuprofen)
 • Iwapo mtoto amerithishwa matatizo ya figo kutoka kwa familia
 • Iwapo mama ana mimba ya mapacha na ikatokea mtoto mmoja ana matatizo ya kiafya hapo itasababisha upungufu wa amniotic acid.

Kwa kawaida mimba inavyozidi kukua, kiasi cha amniotic fluid hupungua hasa kipindi cha  (third trimester)  wiki ya 36-38. Iwapo tumbo la mama litaoneka dogo zaidi kuliko umri wa mimba (miezi au wiki) basi  mkunga (midwife) au daktari anaweza kupima kiasi cha amniotic acid, kwa  sababu hiyo ni dalili mojawapo ya kupungua kwa amniotic fluid.

MADHARA YATOKANAYO NA UPUNGUFU WA AMNIOTIC FLUID

 • Kuharibika kwa mimba( Miscarriage)
 • Kuathiri ukuaji wa mtoto hasa mapafu na misuli.
 • Kusababisha mtoto kugeuza  matako au miguu badala ya kichwa wakati wa kuzaliwa
 • Mtoto anaweza kupata choo chake cha kwanza kabla hajazaliwa (akiwa tumboni) hivyo  kumsababishia kushindwa kupumua vizuri.

USHAURI

Ni muhimu mama kuhudhuria kliniki mara kwa mara bila kukosa, kwa sababu itasaidia kugundua tatizo lolote mapema na kusaidiwa. Iwapo chupa ya maji ikapasuka kabla ya muda au kwa muda muafaka ni vizuri kuwahi hospitali,  sababu amniotic fluid inaweza kupungua na   kusababisha infection kwa asilimia kubwa .

Hivyo ni vizuri kuwahi hospitalini  ili kuangalia utasaidiwa vipi kama ni kupewa  antibiotic kwa ajili ya kumwepusha mtoto na mambukizi n.k . Mama mjamzito jitahidi kunywa maji  kiasi cha kutosha, glasi 8 kwa siku au zaidi ukiweza. Itakusaidia kutopata tatizo la kupungukiwa maji mwilini (dehydration) ambalo ni hatari kwako na mtoto.