
Wakati wa kuwa na mtoto huwa ni kitu cha furaha wakati mwingine kinaweza kuwa ni kitu cha
kuogopesha sana hasa kwa wazazi wa mara ya kwanza. Usiogope wazazi wengine wanafanya vizuri tuu
na hawahitaji kusoma vitu vingi kuhusu watoto, ni sawa unahitaji kujifunza kuhusu watoto na ninashauri
ufanye hivyo ila sio usome kila kitu kama unaanza darasa la kwanza.
Habari nzuri ni kwamba wazazi wengi swala la kumjali mtoto na kumhudumia huwa linakuja
automatically na utajikuta tuu unajua nini cha kufanya kama mtoto akifanya jambo lolote.
Hizi ni baadhi ya tips ambazo unatakiwa kuzikumbuka wakati unamlea mtoto wako wa kwanza
Jiamini na ufanye unavyoelewa
Kama upo katika ile hali ambayo hujui nini cha kufanya, basi jiaminii na ufanye kile ambacho unaona ni sawa kukifanya kwa wakati huo. Utakuja kushangaa idadi ya vitu ambavyo umeweza kuvifanya hata katika wakati mgumu. Jua kwamba utafanya makosa hapa na pale: kila mzazi anafanya makosa ila cha ajabu ni kwamba pamoja na hayo makosa bado wazazi wanahakikisha mtoto yupo salama mda wote, wazazi wanajifunza kutokana na makosa Ni muhimu kujua kwamba hauko sawa katika kila kitu so kuna sehemu utakosea alafu utajifunza baada ya hapo utaelewa kila kitu.
Kuwa na mtu wa kukusaidia. :
Kama ni ndugu yako au rafiki yako itakua vizuri ukiwa na mtu wa namna hii ili akusaidie katika hali ambazo utahitaji msaada na sehemu ambazo hujui nini cha kufanya. Kila mtu ana mtu ambaye anaweza kumuita wakati anahitaji msaada.
Kuwa na dakitari wako unayemuamini
Kama utaku unahitaji dakitari maalumu kwa ajili ya mtoto wako basi hili ni wazo zuri tafta dakitari
maalumu ili aweze kukusaidia katika kufanya maamuzi sahihi. Hii ni kitu muhimu kwa sababu itafikia
kipindi ambacho mtoto wako anaweza kuumwa na hutokua na mtu ambaye unaweza kuumuliza na
akakupa ushauri na ukamuelewa so ukiwa na dakitari hapo ni sawa. Hii unaweza kufanya hata kama
huna mpango wa kuwa na dakitari maalumu cha kufanya ni kuchukua mawasiliano ya dakitari yoyote
ambaye unamuamini ili likitokea tatizo unamuuliza