Umri Wa Mtoto Kutembea

Watoto wengi kwa hali ya kawaida akishafikisha umri wa miezi 9 mpaka 12 huwa ndio wanaanza kutembea na akishafikisha umri wa mwaka mmoja na miezi miwili au miezi mitatu kwa kawaida anatakiwa awe anatembea vizuri. Ila usijali kama mtoto wako atachelewa kutembea maana kuna watoto wengine wanaweza kuanza kutembea akishafikisha umri wa mwaka moja na miezi saba au nane. Mtoto katika mwaka wake wa kwanza anakua busy kukua jinsi ya kucontrol mwili wake na akili na mishipa yote ya mwili ndio inakua inakomaa, kwa hiyo ataanza kujifunza kubilingita, kutambaa kabla hajaanza kusimama na hatimaye kutembea.

 

Sasa kuanzia hapo kitu kinachokuwa kimebaki ni kujiamini yeye mwenyewe na kuwa na balance ya mwili wake. Siku moja kama mtoto wako akisimama kwenye kochi hiyo ni hatua nzuri.

 

Mtoto Anajifunzaje Kutembea.

Miguu ya mtoto wako anapozaliwa inakua haina nguvu za kuubeba mwili wake wote, ila kama ukimbeba na kumsimamisha huku unamshikilia mikono anaweza kuanza kuisimamia miguuu taratibu na kuanza kujaribu kukanyaga chini kwa nguvu kama vile anakua anatembea. Hii huwa ni hatua ya kwanza na anaweza kuifanya kwa mda wa miezi kadhaa.

 

Mpaka mtoto wako akishafikisha umri wa miezi sita anaweza kuanza kusimama kidogo kwa sekunde kadhaa  alafu anadondoka chini na kama ukiwa unamshikilia taratibu basi hili linaweza kuwa ni zoezi zuri la kumsaidia mishipa ya miguu yake kukomaa na kuendelea kukua wakati anaendelea kujifunza jinsi ya kucontrol mwili wake hapo akiwa anatambaa na kukaa.

Mtoto wako akishafikisha umri wa miezi 9 anatakiwa basi awe anaweza kusimama mwenyewe angalau kwa kushikilia kochi au kitu chochote cha kumsaidia, au kama ukimshikilia kidogo tu na kumpa support anaweza kusimama mwenyewe na kutembea.

Baada ya kufikisha miezi 9 na 10 mtoto wako ataanza kujifunza jinsi ya kukunja miguu na magoti na jinsi ya kukaa na kusimama na ni kitu ambacho huwa ni kigumu kuliko unavyofikiria ila kwa uangalizi wako anaweza kufanikisha.

Baada ya kuwa anaweza kuucontrol mwili wake hapo akifikisha mwaka mmoja basi hapo atakuwa anaweza kutembea hata kukimbia. Hapa ataanza kuwa anaweza kutoka sehemu moja kwenda nyingine japo mwanzo hatokua anaweza kutembea mwenyewe kabisa ila katika umri huu anakua atleat vizuri ila watoto wengi akishafikisha umri wa mwaka mmoja na kuendelea anakuwa anaweza kutembea mwenyewe.

Kama mtoto wako akifikisha mwaka mmoja na unaona hana dalili hata za kusimama mara nyingine huwa ni sawa kuna baadhi ya watoto wanachelewa kidogo ila kama akifikisha umri wa mwaka mmoja   na miezi saba au miaka miwili nabado unaona hawezi kusimama wala kutembea hatua kadhaa basi ni vema akumpeleka hospital wakamchunguze

Kitu cha mwisho ambacho unatakiwa kukumbuka kama mzazi ni kwamba, ukishagundua tuu mtoto wako anaweza kuanza kutoka sehemu moja mpaka sehemu nyingine iwe ni kwa kutambaa au kutembea, basi unatakiwa uanze kuweka usalama wake mbele kwanza. Hii ni kuhahakisha hauachi vitu vya hatari mbele yake unapotaka kumuacha, au kama kuna ngazi please usimuache mtoto karibu na ngazi maana utasikia tu akashafika chini na hajitambui, ndoo za maji zifunike, la sivyo utajikuta unadeki nyumba nzima, pasi kama umemaliza kunyoosha itoe hapo sebuleni, kama kuna nyaya za umeme zipo wazi huo ndio mda wa kuita fundi aje azirekebishe.