Umri Wa Mtoto Kutambaa

umri wa mtoto kutambaa

Kutambaa huwa ni njia ya kwanza kwa mtoto kuzunguka na kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine.

kwa kawaida ataanza kujifunza kubalance mikono yake na magoti, baada ya hapo ataanza kujua jinsi ya kwenda mbele na kurudi nyuma kwa kusukuma magoti yake, wakati huo huo anakua anajihimarisha mishipa yake ambayo itamsaidia kutembea baadae.

 

Lini Mtoto Anaanza Kutambaa

Watoto wengi huwa wanaanza kutambaa wakifikisha umri wa miezi saba. Hapa ndio utundu wa kuzunguka zunguka huwa unaanza, na zile harakati za kutaka kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine huwa zinaanza.

umri wa mtoto kutambaa

Njia Za Kumsaidia Mtoto Kutambaa

Kila mtoto anazaliwa na style yake kwa hiyo unaweza kukuta mtoto wako wala hata haonyeshi dalili za kuanza kutambaa, kwa hiyo kitu ambacho unaweza kufanya ili kumsaidia mara moja moja jaribu kumlaza awe kama amelalia tumbo kwa dakika kadhaa alafu uone kama atakua anajaribu kutumia mikono yake kunyanyuka. Kitendo cha dakika mbili au tano, ila kinaweza kumsaidia kidogo kugundua kuwa anaweza kutumia mikono kunyanyuka.

Njia nyingine ni kuweka vitu ambavyo anapenda kuchezea kwa umbali kidogo ili uone kama anweza kujisogeza mwenyewe. Hii njia ni nzuri kwa kumfundisha mtoto wako kuanza kutambaa, maana kwa mfano kama unaona analilia mdoli we uweke mbali kidogo ambapo atatakiwa kujisogeza kidogo ili kuugusa alafu mwambie aje, kwa hiyo kwa kuwa anakitaka sana atajaribu kujisogeza na hapo ndio atazidi kujifnza zaidi na zaidi.

Kitu cha mwisho ambacho unatakiwa kukumbuka kama mzazi ni kwamba, ukishagundua tuu mtoto wako anaweza kuanza kutoka sehemu nyingine mpaka sehemu nyingine iwe ni kwa kutambaa au kutembea, basi unatakiwa uanze kuweka usalama wake mbele kwanza. Hii ni kuhahakisha hauchi vitu vya hatari mbele yake unapotaka kumuacha, au kama kuna ngazi please usimuache mtoto karibu na ngazi maana utasikia tu akashafika chini na hajitambui, ndo za maji zifunike, la sivyo utajikuta unadeki nyumba nzima.

Good luck na kama utakuwa na swali lolote please follow account yetu ya intagram then uliza swali… Cheers