Uji Wa Mchele Kwa Watoto Kuanzia Miezi Sita

Uji ni lishe nzuri kwa watoto waliofikisha miezi sita na kuendelea! Mzazi unatakiwa umpikie uji wa aina tofauti ili asikinai mapema, sababu utakapo mpa uji wa aina moja lazima atauchoka na kuukataa!

Unaweza tumia nafaka tofauti kutengeneza uji , Taasisi ya afya na lishe wanashauri   mtoto alie chini ya miaka 5 hawezi tengenezewa nafaka nyingi kwa pamoja ,nafaka zisizidi  mbili mfano mahindi na mchele au ukamsagia mahindi peke ikawa moja.

Uji Wa Mchele

Jinsi ya kuandaa uji wa mchele

Muda – Dakika 30

Mahitaji

  • Mchele robo kikombe
  • Apple 1
  • Ndizi mbivu 1 (iliyoiva tayari kuliwa)
  • Siagi/butter kijiko 1 cha chai
  • Nutmeg (Kungumanga) robo kijiko – inamsaidia mtoto kwenye ukuaji wa ubongo.
  • Maziwa kikombe 1

Jinsi Ya Kupika.

Pembua na kusafisha mchele kwa Maji safi weka kwenye sufuria na katia vipande vidogo vidogo vya apple hakikisha umelimenya kabla ujaweka.

Ongezea ️maji kikombe 1 funika weka na nutmeg bandika jikoni moto usiwe mkali baada ya dakika 25 epuwa kikiwa kimeiva.

Wacha kipoe weka Kwenye blenda ,ongezea ndizi mbivu 1 na maziwa pamoja na siagi saga kwa pamoja . Usitumie sukari ndizi ndio unaitumia kama sukari.

Kitakuwa tayari kuliwa baada ya kupoa.

Kungumanga inafaida nyingi mwilini, wengi wanatumia kwenye vyakula vyenye sukari, ila usimwekee nyingi kipimo ni robo kijiko kwa mtoto ukimpa nyingi itamfanya alale sana.