U.T.I Kipindi Cha Ujauzito(URINARY TRACK INFECTIONS)

Urinary Tract Infection (U.T.I) ni ugonjwa unaowasumbua wanawake wajawazito mara kwa mara. Ugonjwa huu hushambulia kutokana na mazingira tofauti.Haswa maeneo yenye hali ya hewa ya joto inawaadhiri zaidi.

U.T.I NI NINI

Ni kifupi cha maneno’ Urinary Track Infection’. Ni ugonjwa ambao unashambulia njia ya haja ndogo(mkojo). Ugonjwa huu hushambulia mfumo mzima wa mkojo hususan  mirija ya mkojo (ureter)  na kibofu cha mkojo .

 

CHANZO CHA U.T.I

Ugonjwa wa U.T.I hutokana na virusi kutoka kwenye ngozi yako, sehemu ya uke na sehemu ya haja kubwa. Virusi hivi vinapanda kutoka chini (ukeni) na  kwenda  kwenye mfumo wa mkojo na kusababisha maambukizi . Tunashauriwa  baada ya kuoga au tunapojisafisha baada ya kujisaidia , tuanzie mbele (ukeni) kurudi nyuma (njia ya haja kubwa)  vinginevyo tunasambaza bakteria zinazoleta ugonjwa.

DALILI ZA U.T.I

Mara upatapo maumivu ya ghafla kwenye  njia ya mkojo àu figo ni vizuri ukawahi kumwona daktari. Maumivu huambatana na dalili zifuatazwo:

 •  Homa kali
 • Maumivu ya mgongo
 • Maumivu chini ya mbavu au chini ya kitovu
 • Kichefuchefu na kutapika

 

Kushikwa na hamu ya kukojoa ila mkojo hautoki au kutoka kidogo kidogo sana

 • Unaweza kutokwa na damu au usaha.
 • MKojo huwa na harufu kali na rangi kubadilika na inaweza ambatana na damu
 • Maumivu wakati wa kushiriki tendo la ndoa

 

AINA ZA U.T.I

 • Cystitis or Bladder infection – Mara nyingi bakteria wanakusanyika kwenye kibofu na kusababisha uvimbe. Kwa kawaida ugonjwa huu huwashambulia zaidi  wenye umri wa kujamiiana  mathalan  kati ya miaka 20 – 50 .
 • Maambukizi ya figo – bakteria wanawea kupita kutoka kwenye kibofu kupitia mirija ya mkojo (ureter) na kuathiri figo moja au yote mawili, ugonjwa unaojulikana kama ‘ pyelonephritis’. Ugonjwa huu unawaathiri sana wajawazito na huweza kusambaa kwenye damu. Madhara huwa makubwa kwa mama mjamzito na huweza kusababisha mtoto kuzaliwa njiti.
 • Asymptomatic bacteriuria –  Mara nyingine bakteria katika njia ya mkojo hawaonyeshi dalili zozote.

 

TIBA

 • Kunywa glasi 8 za maji kila siku
 • Kila mara jifute kuanzia mbele (ukeni) kuelekea nyuma kuzuia kusambaza bakteria.
 • Hakikisha unajisaidia haja ndogo mara  kabla na baada ya tendo la ndoa
 • Tumia kilainishi aina ya kimiminika unapojamiiana, pale inapobidi kufanya hivyo.
 • Epuka kutumia vipodozi au sabuni kali zinazoweza kukusababishia michubuko
 • Jisafishe sehemu za siri na maji ya uvuguvugu kabla ya tendo la ndoa.
 • Vaa chupi za pamba ni nzuri kupitisha hewa kwa urahisi
 • Epuka kuvaa chupi za kubana.
 • Kunywa maji ya madafu au nazi glasi 2 kwa siku
 • Kula matunda nanasi,machunwa,matikiti maji ,nyanya kwa wingi
 • Unaweza kutafuna kitunguu saumu punje 3 kwa siku
 • Tumia mtindi kwa wingi inasaidia kuuwa wale bakteria wanaokushambulia
 • Epuka kutumia choo kichafu
 • Epuka kula na mojo muda mrefu
 • Kuna tiba ya dawa za antibiotic kuangazimiza bakteria kwa haraka.

 

U.T.I NI HATARI PIA KWA MAMA MJAMZITO

Mama mjamzito ni rahisi kupata U.T.I kwa sababu mirija  ya mfumo wa mkojo inakuwa imebanwa zaidi kipindi cha mimba na hapo kuzuia  mkojo ukapita kwa urahisi,ndipo bakteria wanapata nafasi ya kuzaliana kwa urahisi kwa kushambulia urethra .

 

Mama anapopata maambukizi husikia dalili kama hizo milico orodhesha hapo juu zinaweza zikaongezeka zaidi kama

 • Kupata maumivu wakati wa kushiriki tendo la ndoa
 • Maumivu ya nyonga na au chini ya tumbo

 

MADHARA YA UTI KWA MAMA MJAMZITO

 • U.T.I inamwadhiri mtoto haswa kwenye ukuaji wake unamdhoofisha afya yake na kuwa na uzito mdogo
 • Mtoto anakosa nguvu hivyo mama anashindwa kusikia mama mtoto anacheza tumboni
 • Kuna dalili kubwa ya mtoto kuzaliwa njiti(pre mature)
 • Kuharibika kwa mimba (miscarriage)

 

USHAURI

Wanawake wanatakiwa kuepuka kuweka kuweka vidole ukeni wakati wa kutawaza na kutokutoa ule ute mweupe  kwani ule ndio kinga yako kubwa kuepuka mambukizi haswa kama U.T.I.

Unachotakiwa kufanya wakati wa kuoga ni kujimwagie maji  kwa nje ya uke na usitumie sabuni kali au shampoo kwani zinauwa bacteria wazuri wanaokupa kinga . Unapotumia choo cha public kuwa makini na usafi wa mazingira ya choo na maji utakayo tumia kunawa.