Toa Weusi Wa Kwapani(Black Armpit) Kwa Njia Asilia

Weusi chini ya kwapa sio ugonjwa ni mabadiliko ya ngozi  unapata watu wengi  na kuwafanya wasiwe comfort kuvaa nguo za wazi mbele za watu ,Kupatwa kwa weusi makwapani una sababishwa na kunyoa mara kwa mara,ngozi kupata dead cells ,mtu anapotumia  deudorant yenye alcohol hubadili rangi, matumizi ya creams za kunyolea( kupakwa makwapani),kutokwa majasho mengi makwapani,kuvaa nzuo nyingi au nzito na mwili kukosa hewa vizuri husababisha kupata weusi kwapani.

 

image

Home remedies

Unaweza ukatoa  weusi kwa kutumia vitu halisilia ambayo ni salama na havina chemicals  kama

  • Lemon-chukua limao au ndimu kata vipande duara upake  sukari  au asali kwa juu ,then chukua hivo vipande ujipate makwapani mara 2 kwa siku acha kwa dakika 10 kabla ujaenda kuoga then osha kwa maji vugu vugu ,lemon inatumika kama bleach kutoa iyo rangi na kutoa dead cells kwenye iyo ngozi ya kwapa.

image

 

  • Baking soda-inasaidia kutoa dead cells kwa urahisi ,changanya baking soda na maji iwe nzito nzito paka kwapani acha kwa dk 10 osha na jikaushe fanya hivyo mar 2-3 kwa wiki ,endelea na zoezi mpaka utakaopona umeridhika na mabadiliko.

 

  • Maganda ya machungwa (orange peels) chukua maganda ya machungwa kausha juani yakikauka ponda ,changanya na maji ya rose (rose water)koroga ongezea na maziwa paka kwa dakika 10-20 utaofa ,utaendelea na zoezi .

 

  • Viazi ulaya/mbatata- menya viazi kata vipande jipake makwapani yale maji yake yakiingia kwenye ngozi yanatoa rangi nyeusi au unaweza kuponda kikiwa kibichi na kujipaka kwa dk 10-20 utanawa utafanya hivyo mara 2 kwa siku mpaka weusi utakapo isha.

image

  • Tango ( cucumber)-kata vipande na ujipake kwapani yale maji yake ndio dawa au saga iwe paste ndio upake ikae kwa dakka 10-20

 

  • Sukari -chukua brown sugar changanya na olive oil paka  badaa ya mda osha.

 

  • Mafuta ya nazi-yana vitamini E yanasaidia kung’arisha ngozi paka baada ya dk 10-20 toa na kunawa kwa maji vugu vugu .

 

image

Zoezi hili linaweza chukua mda mchache ukaona mabadiliko makubwa au ikachukua mda mrefu mapaka uone mabadiliko inategemea kila mtu na ngozi yake ,Zingatia kutumia dodoki la kuogea usugulie makwapa na hakikisha hukai na nywele ndefu  makwapani. Tumia hand shaver isiwe kiwembe iwapo umetumia njia hizi kwa miezi 1-2 na hakuna mabadiliko mwone daktari .Kuna badhi ya creams au deudorants nazo zinasaidia kutoa weusi kwapani.