Smoothie Ya Ndizi Na Maziwa Kwa Afya Bora Ya Mtoto

Smoothie ya ndizi na maziwa inavirubisho vingi vizuri mwilini kama protein, fiber, vitamini, madini ya chuma,nk. Huongeza uzito  inakupa nguvu na kulainisha ngozi ya mwili, kujenga mifupa iwe imara na faida nyinginezo nyingi.

Mahitaji

  • Ndizi mbivu 2
  • Maziwa glas 1
  • Test ya vanilla au asali ukipenda!

Jinsi ya Kuandaa

Menya ndizI mbivu, weka kwenye blenda ongezea glasi moja ya maziwa na robo kijiko cha chai cha vanila au asali utasaga pamoja ukipenda, unaweza sagia na vipande vya barafu kwa matumizi ya mtu mzima! Tayari kutumika!

Watoto Chini Ya Miezi 12

Mama utumie maziwa ya kopo au ya kwako baada ya kukamua ili ukisaga utumie, maziwa ya ng’ombe madaktari  hawashuri kupewa mtoto chini ya mwaka mmoja wanauwezo mkubwa wa kumdhuru kutokana na protein nyingi ilipo ndani.