Siri Ya Kumfanya Mtoto Alale Vizuri

Mtoto akilala vizuri ndio anakua na afya njema. wakati watoto wana style tofauti za kulala na mahitaji tofauti basi kuna baadhi ya vitu ambavyo ntakuelekeza unaweza kujifunza na kuvifanyia kazi,

Chagua Mda Mzuri Wa Kulala.

Ni vema kuchagua ni mda gani mzuri kwa yeye kulala. wataalamu wanashuri saa moja au saa mbili ni mda mzuri wa mtoto kulala kama akizidisha hapo basi anaweza sumbua kidogo kulala.

Fuata Mda.

Ukishachagua mda wa kumlaza mtoto ni vema ukawa unaufata mda huo wa kulala kwa sababu ukiendelea kufanya hivyo mtoto wako ataanza kuzoea huo mda na kwa sababu hiyo basi atakuwa hasumbui wakati wa kulala.

 

Muandae Mtoto.

Watoto wadogo wanatakiwa kuandaliwa mapema kabla ya kwenda kulala. Kuna ile njia ambayo wakina mama wengi wanaitumia, kuwa mtoto kabla hajalala kwanza anaoga, pili unampa chakula au kama ni maziwa na kisha unamlaza analala. Kwa hiyo kama unataka mtoto wako alale saa mbili basi saa moja  na nusu unaanza kumuandaa mapema ili iwe rahisi kwake kulala.

Mtoto alale

Mpeleke Kitandani Kabla Hajasinzia

Hii ni kwamba inatakiwa wakati mwingine umlaze mtoto kitandani kabla hajasinzia kabisa, hii ni kwa sababu anatakiwa kujifunza kulala mwenyewe na kupitiwa na usingizi mwenyewe kuliko akiwa ameshalala ndio unamlaza kitandani, kwa hiyo kwa kumpeleka kitandani kabla hajasinzia kabisa unakua pia unamfundisha jinsi ya kujilaza mwenyewe, maana sisi tunautaratibu wa kumbeba mgonogni mpaka anasinzia ndio maana unakuta mtoto amekula vizuri ila kulala mpaka umuweke mgongoni wakati unaweza kumlaza kitandani ajifunze.

 

Acha Tabia Ya kumlisha kama njia ya Kumlaza.

Hii ni njia wakina mama wengi huwa wanaitumia. Yaani unakuta mama anatumia njia ya kumyonyesha mpaka analala. Wakati mwingine kwa kweli huwa inasaidia maana ndio inamfanya mtoto analala ila kuna wakati mama unatakiwa kuacha hii tabia. Mtoe mtoto wako hapo muweke kitandani ajifunze kulala mwenyewe, inasaidia sana kama ukianza kumfundisha mtoto wako kulala mwenyewe na sio mpaka uwe nae karibu mda wooote

Kuna wakati mtoto anaweza kuwa amechoka saana kwa hiyo unakuta anachelewa kulala, kwa hiyo jinsi ya kudeal na mtoto wa aina hii jaribu kumpeleka mtoto wako kitandani mapema kabla ya mda wa kulala ili asichoke sana na kutumia mda mwingi akiwa macho.