Saratani Ya Shingo Ya Kizazi (CERVICAL CANCER)

Saratani ya shingo ya kizazi (cervical cancer) ni ugonjwa unaowapata wanawake. Seli inaleta mabadiliko ya mfumo wa chembechembe zilizopo kwenye mfumo wa shingo ya kizazi kushamiri ,kukuwa , kuzaliana kwa kasi na kuharibu mpangiliano wa maumbile.

Matokeo yake yanakuwa zaidi na kujitokeza nje ya mfuko wa uzazi  hiyo hali siyo ya kawaida kiafya. Saratani ya shingo ya kizazi ni moja kati ya saratani zinaongoza kusababisha vifo vingi vya wanawake duniani.” Squamous cell carcinoma” ndio saratani inayosumbua wanawake wengi  duniani kwa asilimia 20.

Mwaka 2010  shirika la afya duniani (W.H.O)Ilionyesha ripoti yaTanzania kwa idadi ya wathirika wa saratani ya shingo ya kizazi ikaonyesha wanawake 6241 huugua saratani ya shingo ya kizazi kwa mwaka na kati yao  wanawake 4,355 hufariki kwa mwaka. Wathirika wakubwa wapo kati ya umri wa miaka 15 mpaka 44 na  takribani  asilimia 33.6 inaonyesha walioathirika wamesababishwa na virusi waitwao ”Human Papillomavirus” (HPV) .Wanawake weusi yaani wakiafrika ndio wanaongoza kwa kushambuliwa na saratani ya shingo ya kizazi duniani kutokana na tafiti za Shirika la Afya Duniani (W.H.O)

PICHA INAONYESHA JINSI CANCER YA KIZAZI INAVYOSHAMBULIA

Visababishi vya saratani ya kizazi

Maambukizi ya virus vya human papilloma  ndio yanayosababisha saratani ya shingo ya kizazi. Kuna zaidi ya aina 150 ya virusi hivi vya human papilloma , ambapo aina tatu (yaani aina ya 26,53,66) ndio venye hatari sana ya kusababisha ugonjwa huu, aina ya 16 na 18 ndivyo vinavyojulikana kusababisha zaidi ya asilimia 70 ya ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi. Virusi hivi huambukizwa kwa njia ya kujamiana au kugusana kwa ngozi ya mtu mmoja na mwingine, na huambukiza wanaume kwa wanawake.

Vyanzo vya saratani ya shingo ya kizazi.

 • Virusi viitwavyo Human papilloma Virus (HVP) ndio chanzo kikubwa cha ugonjwa ambapo  wanaambukiza kupitia ngono(Ngozi kwa Ngozi)
 • Upungufu wa kinga mwilini – Magonjwa yanayosababisha upungufu wa kinga mwilini  ukimwi(HIV) huchangia kupata saratani ya shingo ya kizazi.
 • Matumizi ya madawa makali  husababisha upungufu wa kinga mwilini.
 • Lishe duni au utapiamlo
 • Uvutaji sigara – Kemikali zilizopo kwenye sigara huchanganyikana na seli au chembechembe za shingo ya kizazi hivyo kuleta mabadiliko katika shingo ya kizazi hatimaye kusababisha saratani.
 • Matumizi ya vidonge vya uzazi wa mpango(oral contraceptive pill) vinamweka mwanamke kuwa kwenye hatari ya kupata saratani ya kizazi
 • Kuridhi ugonjwa kutoka kwa familia  – Saratani hii pia inahusishwa na kiashiria cha aina ya HLA-B7 ambacho kinaweza kurithishwa kama kwenye familia kuna historia ya huu ugonjwa.

Kundi lipi lipo kwenye hatari zaidi ya kupata saratani ya shingo ya kizazi

 • Watoto wa kike wanaoanza kushiriki tendo la ndoa wakiwa na umri mdogo. Mabinti wanaoathirika zaidi ni wale wanaoanza kujamiana wakiwa na umri chini ya miaka 18.
 • Mwanamke anapokuwa na wapenzi wengi – mwanamke anaposhiriki tendo la ndoa na idadi kubwa ya wanaume.
 • Ugonjwa wa masundosundo (dalili ni matezi na muda mwingine vidonda katika sehemu ya siri ya mwanamke). Hii husababishwa na virusi vya ‘human papilloma virus’.
 • Wanawake wanao zaa  idadi kubwa ya watoto  –  wako kwenye hatari ya kupata saratani ya shingo ya kizazi.
 • Umri  wa mwanamke unavyozidi kuongezeka ndivyo hatari ya kupata saratani inavyoongezekaWanawake wenye zaidi ya miaka 45 wako kwenye hatari zaidi ya kupata saratani ya shingo ya kizazi.

 

Dalili za saratani iliyosambaa ni kama zifuatavyo;

Saratani ya kizazi inaweza kuonyesha  dalili moja kwa moja au inaweza isionyeshe dalili zozote .Zifuatazo ni baadhi ya dalili :

 • Maumivu ya tumbo chini ya kitovu
 • Kutokwa na maji maji yanayotoa harufu mbaya ukeni kwa wingi (vaginal discharge)
 • Kutokwa na damu nyingi ukeni
 • Kupata maumivu wakati wa kushiriki tendo la ndoa na kutoka damu.
 • Maumivu ya mgongo na  uchovu mwilini

Saratani  inaposhamiri  mgonjwa husikia dalili zifuatazo:

 • Kushindwa kubana mkojo hivyo  huweza kujikojolea
 • Kuvimba mguu moja
 • Kupungukiwa na uzito na kukosa hamu ya kula
 • Kubadilika rangi ya kinyesi  upatapo haja kubwa
 • Kuishiwa nguvu,
 • Maumivu ya mifupa.

Mgonjwa anapochelewa kutibiwa saratani inazidi kusambaa sehemu nyingine za mwili haswa sehemu za tissue na organs kama figo,ini,mapafu ,mifupa,kibofu cha mkojo nk.

Vipimo vya saratani ya shingo ya kizazi

Unapoona  dalili hizo ni vizuri uwahi kituo cha afya na kufanyiwa vipimo . Kuna Aina nyingi za vipimo kulingana na hatua ugonjwa  ulipofikia. Baadhi ya vipimo ni:

 • Pap Smear ni kipimo kinachochukuliwa toka kwenye mfuko wa kizazi, kwa kutoa seli kuangalia kama zina mabadiliko
 • Cervical Biopsy – Kipimo hiki huhusisha uchukuaji wa nyama kutoka kwenye mwili. Inashauriwa kufanya kipimo hiki angalau mara moja kwa mwaka ili kujua afya yako.
 • Cervical Biopsy – Kipimo hiki huhusisha uchukuaji wa nyama kutoka kwenye uvimbe katika shingo ya kizazi na hupelekwa maabara kuchunguzwa kama kuna saratani au la. Kipimo hiki kinathibitisha uwepo wa saratani.

 

Colposcopy – Hii ni aina ya darubini inayotumiwa kuchunguza saratani ya shingo ya kizazi ili kuangalia kama kuna tishu ambazo si ya kawaida.

 • Cone Biopsy – Kipimo hiki hufanywa kwa kuchukua nyama kutoka katika shingo ya kizazi.
 • Picha ya kifua ya X-ray – Kuangalia kama saratani imesambaa kwenye mapafu au bado.
 • CT Scan – Kuangalia kibofu cha mkojo kama kimeathirika au la, na pia kuangalia kama saratani imesambaa kwenye mifupa, ini, figo na sehemu nyingine za mwili.

Makundi ya saratani ya shingo ya kizazi

Saratani ya shingo ya kizazi imegawanyika katika hatua mbali mbali kulingana na TNM ama FGO (Classification) kama ifuatavyo;
Hatua ya 0 – Saratani iliyo kwenye chembechembe au seli za aina ya epithelium lakini haifiki kwenye nyama za ndani za shingo ya kizazi.
Hatua ya 1 – Saratani iliyopo kwenye shingo ya kizazi.
Hatua ya  2– Saratani iliyosambaa hadi kwenye utupu wa mwanamke sehemu ya juu kwa sehemu  2/3.
Hatua ya 3 – Saratani iliyosambaa hadi kwenye ukuta wa nyonga na sehemu ya chini ya uke kwa 1/3. Hii inaleta madhara katika figo.
Hatua ya  4 – Saratani iliyosambaa hadi nje ya utupu wa mwanamke na pia husambaa hadi kwenye sehemu nyingine za mwili kama mapafu, figo, mifupa n.k.

Tiba

Tiba ya saratani  inategemea na kundi na aina ya saratani mgonjwa aliyonayo. Saratani ya kizazi inatibika iwapo mgonjwa atakuwa hajashambuliwa sana na virusi vya papillormasivirus.

 • Tiba ya mionzi ya radiotherapy  inatibu saratani ya awali -hapa mgonjwa atafanyiwa upasuaji kutoa sehemu ya kizazi iliyoathirika   kwa njia ya kuunguzwa na  mionzi .
 •  
 • Tiba ya dawa (chemotherapy) ni tiba anayopewa mgonjwa ambae saratani ya kizazi imeshamwathiri kwa kiasi kikubwa.   Hapo  inatakiwa kuiondoa moja kwa moja au kuipunguza makali isiweze kusambaa sehemu nyingine za mwili.  Kwenye  tiba hii ya chemotherapy zipo aina tofauti   kulinga na aina ya saratani ulio nayo. Kuna kumeza dawa za aina moja (monotherapy) zinazoenda kuuwa chembechembe au seli za saratani. Njia nyingine ni ya kuchoma sindano kupitia mishipa.
 • Tiba ya mionzi ya (Radiation therapy) ya x-ray inayouwa seli za saratani.
 • Tiba ya upasuaji (surgical treatment)  hi imegawanyika sehemu 3 toafuati.
 • Tiba upasuaji (surgical treatment) – Aina za upasuaji kwa mgonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi ni kama zifuatazo;
  Cryosurgery – Mpira maalum (probe) huingiziwa kupitia kwenye uke  hadi kwenye shingo ya kizazi na majimaji ya nitrogen hupitishwa yaliyo na baridi ya nyuzi joto -160 0 celsius yenye uwezo wa kugandisha na kuharibu seli za shingo ya kizazi hivyo kuzuia saratani
 • Laser surgery – Aina hii ya upasuaji inatumia mionzi ya laser ambayo huchoma seli za shingo ya kizazi ambazo haziko kwenye hali ya kawaida, mionzi hii haiharibu tishu za pembeni na hutumiwa kwa matatizo ya shingo ya kizazi kabla hayajawa saratani.
  Cone biopsy – Kama nilivyoeleza kwenye vipimo hapo juu.
 • Simple hysterectomy – Hii inahusisha kuondoa mfuko wa kizazi (uterus) kupitia sehemu ya tumboni au kupitia ukeni kwa wagonjwa wa hatua ya  I (Stage I). Madhara yake ni ugumba, kuvuja damu, kupata madhara sehemu ya haja ndogo au utumbo na maambukizi kwenye kidonda.
 • Radical hysterectomy – Hii inahusiha kuondoa mfuko wa uzazi kupitia kwenye tumbo pamoja na tishu za mfuko wa uzazi, sehemu ya juu ya uke wa mwanamke, na tezi za kwenye nyonga. Mayai (ovaries) na mirija ya uzazi yanabakizwa. Madhara yake ni kama ya hapo juu pamoja na kuleta karaha na maumivu wakati wa kujamiiana.
 • Pelvic exenteration – Huhusisha uondoaji wa kibofu cha mkojo, uke, puru (rectum) na sehemu ya utumbo mpana (colon). Upasuaji huu hutumiwa kwa wagonjwa wenye  saratani iliyojirudia.

UTAJIEPUSHA VIPI NA SARATANI YA KIZAZI

Kukwepa huu ugonjwa ni ngumu ila unaweza ukajitoa kwenye hatari ya kuupata kwa kuacha au kufanya vitu vifuatavyo:

 • Usifanye ngono zembe ,tumia kondom itakukinga kupata maambukizi kila unapojamiiana ili kuepuka virusi wa human Papillomavirus ambao ni rahisi kukuletea saratani ya kizazi
 • Mwanamke anatakiwa awe na mpenzi mmoja na hata mwenzako (mwanaume) nae awe na mpenzi mmoja tu,  ili kuepuka saratani ya kizazi
 • Cervical screening -kila mwanamke mwenye umri wa miaka kati ya 25-49 ni vizuri afanye hivi vipimo ili kujua kama ameadhirika au laa!  Kipimo hiki anatakiwa afanye kila baada ya miaka 3.Wanawake wa miaka 50-64 wao wanatakiwa kufanya kila baada ya miaka 5.
 • Acha matumizi ya sigara  na au bangi
 • Acha kuweka vitu vya ajabu ukeni kama ,asali,pamba,marashi,chocolate au peanut butter.
 • Acha kutoa  maji maji ya ukeni wakati wa kuoga ,hayo maji maji  ndio kinga yako inayokuepusha na magonjwa ya kuambukiza, unapoitoa ni rahisi wewe kupata maambukizi sababu huna kinga yoyote.Ukioga jimwagie maji kwa nje tu inatosha uchafu wowote ule unajitoa wenyewe kwa njia ya kawaida.
 • Tumia chanjo ya Gardasil kwa kuzuia saratani ya kizazi (ulizia vituo vya afya) kati ya umri wa miaka 12-26