Sababu Zinazosababisha Mama Mjamzito Kuzaa Mtoto Njiti

Mama mjamzito anapozaa mtoto kabla ya wakati  wake wiki 37, huyo mtoto huitwa Njiti, hii ni kwa sababu anakuwa bado ajafikisha mda wake wa kuzaliwa na mwili wake bado haujakomaa. Watoto njiti wanahifadhiwa kwenye kifaa special kinaitwa (incubator) kinachowapa joto la kutosha kama alilokuwa analipata kwa mama tumboni. Kuna njia nyingine inaitwa Kangaroo mtoto  anabebwa  kifuani kwa mama yake au baba yake akiwa hana nguo ila ataveshwa soksi na kofia na atafunikwa ili apate joto la kutosha ni njia moja wapo ya kumpa joto.

Aina za watoto njiti.

watoto njiti wanakuwa wanatofutiana umri kunawale wanao zaliwa wakiwa na wiki 28- kuna wa wiki 28 -32 baadhi ya watoto wanaozaliwa kati ya wiki hizi wanakuwa wanapata tabu kwenye mfumo wa hewa na (mapafu), kundi la mwisho wanakuwa wanazaliwa wakiwa na wiki 32-37.

Sababu Zipi Zinasababisha Mama Azae Ntoto Njiti.

 • pombe au matumizi ya madawa la kulevya vyote hivyo huchangia mama kuzaa mtoto njiti.
 • Upungufu wa damu mwilini.
 • Uzito mkubwa kwa mama kipindi cha ujauzito.
 • Uvutaji wa sigara au bangi unadhiri .
 • Mama anapokuwa na ugonjwa kama kisukari,pressure ,infections au kifafa cha uzazi .
 • Mama akiwa na matatizo kwenye cervix inashindwa kujifunga na kujikaza kubeba mtoto , kondo(placenta) inapokuwa na tatizo.
 • Mama kushika mimba haraka  baada ya kujifungua mtoto mwingine.
 • Mama anapokuwa na mimba ya (mapacha) anakuwa na hatari ya kuzaa njiti.
 • Chupa kupasuka kabla ya mda wake (,mtoto atabidi azaliwe kabla ya mda Wake).
 • Stress za mama zinaweza mfanya azae kabla ya mda Wake.
 • Kushika mimba chini ya miaka 17 au zaidi ya miaka 35 wanahatari ya kuzaa watoto njiti.
 • Mama asipo uzuria klinik vizuri sababu kunabaadhi ya kipimo atakuwa hapimi, kuna supplements kama za prenatals vitamins au foilic acid zinazomsaidia yeye na mtoto kipindi chote cha mimba anatakiwa atumie,na lishe mbaya ni vyanzo vya kuzaa mtoto njiti.

Dalili Ya Mama Mjamzito Anaetaka Kuzaa Mtoto Njiti

Unapotaka kuepuka kuzaa mtoto njiti lazima mama ujue dalili ni zipi na ukishaziona inakubidi uwahi hospital.

 • Maumivu ya mgongo- utasikia mgongo unauma sana maeneo ya chini maumivu yakuja na kuondoka .
 • Maumivu ukeni kunavuta na kuachia kila baada ya dakika 10 au 20
 • Kutokwa maji maji ukeni kwa wingi.
 • Kutokwa damu inaweza kuwa nyingi au kidogo ukeni
 • Kuhara, kutapika.
 • Maumivu chini ya kitovu.
 • Mtoto kukusukuma kuja chini.(utahisi more pressure kuja chini)
 • Kutokucheza kwa mtoto(mama unatakiwa ufatilie mtoto mapigo yake tumboni ukisikia yupo kimya jaribu kunywa maji , uji,chai au kula chakula atacheza ukaona kimya kinazidi kwa mda mrefu wahi hospitali)

Mtoto Njiti Anakuwa Na Hatari Gani Baada Ya Kuzaliwa

Baadhi ya watoto njiti wanakuwa na hatari ya

 • Kushindwa kupumua
 • Mtoto anakuwa na hatari kupata adhari kwenye ubongo
 • Milango ya fahamu na organs kuadhirika.
 • Wanakua na ukuaji mbaya (afya isiyo nzuri)

Watoto njiti sio wote wanakuwa na afya dhoofu baada ya kukuwa ,wengine huwezi jua kama  walizaliwa njiti kutokana na afya bora walizo nazo. Mama anza klinik mapema ili upewe mafunzo ya kulea mimba pamoja na vipimo muhimu.