Ni Makosa Kupasha Chakula Kwenye Microwaves Kwa Chombo Cha Plastic.

Micro Waves ni mchombo cha umeme chenye( frequence radio Waves )kinachotumika kupashia vyakula. Chombo hiki kinaweza leta madhara iwapo inatumiwa kinyume kama cancer au kuadhiri organs za mwili n.k
Unapotaka pasha chakula tumia chombo cha udongo chenye mfuniko ,vipo vingi vinauzwa special kupashia chakula kwenye microwaves hakikisha umefunika chakula ndio upashe na usiweke kwa mda mrefu utauwa vitamins zilizomo kwenye chakula.

Microwave -safe nazo zinauzwa unaweza ukatumia ni ya material ya glasi!
Tafiti ngingi zimefanywa baada ya kuona tatizo la cancer linazidi ongezeka kwa watoto barani Ulaya n Amerika ,na kugundua chanzo moja wapo ni Microwaves, wazazi wanapasha vyakula kwa kutumia mabakuli ya plastic. Plastic inavyotengenezwa ni mchanganyiko wa Chemicals pale inapopata joto ndani ya Micro Wave huyeyushwa na ile sumu kuingia kwenye chakula inayokuja mwadhiri mtu.
Ushauri tokwa afya bora kwa mtoto
Pasha chakula cha mtoto kutumia jiko,kama chakula kilikuwa kwenye friza kitoe mapema ,wacha barafu liyeyuke weka kwenye sufuria na bandika jikoni ni njia salama zaidi.Maziwa ya mtoto yapashwe kwa kuchemsha maji ya moto pembeni na kisha kudumbukiza chupa ili yapate moyo,usiyachemshe jikoni au kwenye Micro utauwa virutubisho vyote.