Namna Ya Kuhifadhi Maziwa Ya Mama Baada Ya Kupump

Wazazi wanaporudi kazi  baada ya kujifungua,wanajikuta wanaacha kunyonyesha watoto ,kwasababu ya kutokujua kama wanaweza kupump(kukamua)maziwa na kuhifadhi vizuri ,kumwachia mlezi na akampa mtoto  pindi mama yupo kazini. Maziwa unaweza kumpump kwa machine au mkono,mama anaepump maziwa anatakiwa kunawa mikono kabla ya kupump,kuhakikisha mzingira unayopumpia ni masafi na kutumia vyombo visafi kila mara na mama unatakiwa kunywa maji mengi si chini ya glasi 8 kwa siku .

image

Maziwa ya mama yanahitaji kuhifadhiwa vizuri kwa usafi wa hali ya juu kwa kuzingatia muda maalum. mama akikamua  maziwa anaweza hifadhi kwenye jokofu(friji), au nje Ya friji ,kila sehemu unahifadhi kwa kuzingatia muda (masaa)

 

image

 

 NJE YA FRIJI

 Iwapo maziwa ya mama yana hifadhiwa nje ya friji basi uzingatie usafi pale utakapo yaweka utayahifadhi kwa masaa3-4  usihifadhi sehemu yenye joto kali zaidi ya nyuzi joto 25.

 FRIJI

Maziwa yanayohifadhiwa kwenye friji (jokofu)utahifadhi kwa masaa 72 au siku 3,hakikisha chupa imefunga vizuri hewa isipite. Unaweza ukamark chupa kwa kuandika tarehe ya siku ulioweka hayo maziwa Kwenye friji!

Kwenye friza, hapo utahifadhi kwenye chombo safi au storage bags  na kuhifadhi Kwenye friza kwa mda wa miezi 6, ila kwa wale wanaoishi sehemu zenye matatizo ya umeme hii haiwafai. Utaandika tarehe na mwezi ulioweka ili yakiharibika ni rahisi kujua kwa kusoma tarehe. Epuka kuchanganya maziwa yaliokaa mda na maziwa yaliotoka kukamuliwa(fresh)

 

 

JINSI YA KUPASHA MAZIWA YA MAMA

Maziwa ya mama hayawezi pashwa kwa kuchemsha jikoni hapo utauwa virutubisho vyote, unachotakiwa chemsha maji pembeni, weka maziwa kwenye chupa ya mtoto funga na mfuniko dumbukiza iyo chupa kwenye maji moto ulio chemsha acha kwa dakika 3-5 yatakuwa yashapata joto tikisa na tayari kumpa mtoto.

image

Bottle warmer nayo ni nzuri na nirahisi kutumia haina usumbufu unapashia mda wowote au mahali popote penye umeme kwa kuweka maji dumbukiza chupa na kuwasha moto baada ya dakika chache maziwa yanakuwa yashapashwa.

image

 

 

Matumizi mengine ya  maziwa ya mama-unaweza pikia chakula cha mtoto au kusagia pamoja na matunda(smoothie).