Muda Upi Ni Sahihi Kwa Mama Alietoka Kujifunga Kufanya Tendo La Ndoa.

Mama alietoka kujifungua anahitaji kujipa mda ili aweze kushiriki tena tendo la ndoa. Hiii ni kwa sababu kuna uwezekano mkubwa wa kujitonesha kidonda au kufumuka kwa nyuzi kwa wale walio jifungua kwa operation au walio ongezewa njia ukeni.

Mama Aliejifungua Kwa Njia Ya Kawaida.

Njia ya kawaida haina matatizo mengi mama atasubiri baada ya wiki 3-4 akajisikia yupo sawa anaweza kuanza kushiriki tendo la ndoa.

Mama Aliejifungua Kwa C-section (operation)

Unatakiwa kuwa makini sana ongea na mzazi mwanzako, mweleweshane  unahitaji msubirie kidonda kipone kwa ndani na nje ndio muweze kukutana tena kimwili . Utaepuka kujitonesha kwenye milango ya uzazi baada ya wiki 4-6 mshono utakuwa umekauka na kujifunga vizuri hapo unaweza fanya tendo la ndoa.

Kwawale walio jifungua kwa njia ya kawaida wakaongezewa njia nao wanahitaji mda ili kidonda kipone wiki 4-6.

Epuka Mimba Zisizo Tarajiwa.

Mama  kuwa makini utakapo anza shiriki tendo la ndoa ni rahisi sana kupata mimba  tena. Inakupasa kutumia njia za uzazi iwapo hamjapanga kuzaa tena  kama condom n.k. Ni vizuri mkazaa kwa mpangilio. Baada ya wiki 6  kjifungua mama anahatari kubwa ya kushika mimba tena kwa urahisi, japo unaponyonyesha unapunguza kiasi cha  kushika mimba ila sio kwa 100%.