Muda Sahihi Wa Kufanya Mazoezi Kwa Mama Alitoka Kujingua Kwa Upasuaji,Njia Ya Kawaida

Mazoezi ni muhimu kwa afya  ni vizuri mama akafanya baada ya kujifungua itamsaidia mwili wake kurudi  na kuwa na nguvu kwa haraka,kupunguza uzito wa uzazi.Ila mama anatakiwa kuzingiatia hali ya afya  yake ,asifanye mazoezi mazito kwa haraka .

 

Mwili bado unahitaji kupumzika na kupata nguvu zaidi ,ila mazoezi ya kutembea ni mazuri zaidi baada ya siku moja au mbili kujifungua inakusaidia kuepuka kuganda kwa damu (blood glot), kufanya mzunguko wa damu Uwe mzuri na kusaidia kidonda kipone kwa haraka kwa walio jifungua kwa operation au njia kawaida.

C-section

Mama baada ya kujifungua anatakiwa kuwa makini na mshono ili usifumuke kwa kuepuka kufanya kazi nzito,kubeba vitu vizito. Mazoezi aanze baada ya wiki 8-10 baada ya  mshono kukaguliwa na mkunga au daktari na kuona una hali nzuri .

 

Mazoezi fanya  mepesi ya kujinyoosha mwili(stretching),kutembea mwendo mrefu mara mbili kwa siku kwa dakika 30 (asubuhi na jioni).Utakapoona sasa mshono wako umekaza na kidonda kimepona ndio unaweza fanya mazoezi ya kukimbia,kuruka kamba,kuogelea,au kubeba vyuma vizito (gym)

Kujifungua kwa njia ya kawaida.(normal vaginal delivery)

Mama aliejifungua kwa njia ya kawaida anaweza anza mazoezi baada ya wiki 4,iwapo kajisikia amepona na ana nguvu ,ataanza na mazoezi mepesi kama kutembea,stretching,push-up,aerobic dance(utaipata you tube).