Mtoto Hataki Kulala

MTOTO Hataki kulala

Tatizo la mtoto kuamka usiku  wa manane na kukataa kurudi kulala huwa ni jambo la kawaida na hapa ndio wazazi wengi huwa wanapata stresss sana kwenye hili swala. Yaani unakuta mtoto akiamka saa saba tu yaani huyo ndio mpaka saa moja asubuhi. Kitu nichoweza kukwambia ni kwamba hii tabia haitakuwepo milele na itafikia mda mtoto atakua analala kama kawaida ila kuna tips ambazo unaweza kuzifanya ambazo zitakusaidia atleast kupunguza tatizo hili,

 

  1. Watoto pia huwawanapenda mwanga wa mchana.

Wakati wa mchana mwili wa mtoto huwa unahitaji kutofautisha kati ya mchana na usiku ndio maana inashauriwa kuwa kama mtoto akiwa ndani ya nyumba ni  vema kufungua madirisha ili mwanga uingie au kama ni kumtoa nje mtoe apate hewa na mwanga wa kutosha. Kwa mfano kama unamnyonyesha kaa hapo kibarazani.

 

  1. Kama hamna kitu kingine kinachomsumbua basi kitu kingine cha kuangalia ni mazingira anayolala. Je chumba ni kina giza sana?kuna baridi, joto kali, je kuna wakati unamsumbua, watoto wengine wanaamka tu pale wazazi wanapoanza kuongea. Kama ni sahihi basi ongeeni taratibu na kama inawezekana muwekeni kwenye kitanda chake ili asisumbuliwe.

 

  1. Kama mazingira anayolala ni mazuri basi angalia jinsi unavyomlaza. Labda ndio mda wa kumsaidia kujilaza  yeye mwenyewe. Kwa hiyo kama ameamka na hamna kitu kinachomsumbua mwache kidogo tuone kama atarudi kulala yeye mwenyewe, ila kama umeona hana dalili ya kurudi kulala na analia tuu, basi mama ujue ndio ameshaamka mwenzio.

 

Njia za Kumfundisha Mtoto Kulala.

Kuna baadhi ya njia ambazo unaweza kutumia kumfundisha mtoto kulala na njia moja wapo ni kumlaza kitandani au kwenye kitanda chake badala ya kumbeba mgongoni au mkononi, maana ukiendelea hivyo basi unakuta anazoea kulala ni mpaka abebwe so njia nzuri ni kuanza kumzoesha kulala moja kwa moja kwenye kitanda. Kama ukiona analia sana au halali basi myanyue kwenye mkono kwa mda ili atulie alafu mrudishe tena kitandani.

 

Kama unakitanda kile cha watoto ambacho kina bembea basi hapo utakua umemuweza. Kila mara mlaze kwenye hicho kitanda na kisha muache, ukisikia tu anaanza kulia basi kisukume kama awe anabembea na hiyo itamfanya arudi kulala tena na hii ni njia nzuri ya kutoa tabia yake ya kutaka kubebwa kila anapoamka na vile vile haitakupa kazi sana hata wewe.