Mtoto Ameanguka Toka Kitandani Je Nini Cha Kufanya

Hivi umeshawahi kuwa ndani unafanya mambo yako  gafla ukasikia PUU! hata kabla sekunde haijaisha unasikia mtoto anatoa kilio cha HATARI sanaa?? Yaani hapo nahisi utakua ushajua nini kimetokea

 

Kama mtoto wako ameanguka kutoka kitandani mpaka chini, kwenye ngazi au kochi unaweza jiona ni mjinga kiasi gani  unaweza jisahau kumwangalia mtoto mpaka akaanguka! Ila ni jambo la kawaida kwa watoto kuanguka sababu ni wepesi sana ndani ya dakika chache tu anaweza anguka.

Pale mtoto anapofika miezi 3 na kuendelea kama mzazi unatakiwa kuwa makini zaidi, mana anaanza kujifunza kujigeuza geuza akiwa kitandani na sehemu nyingine.

Haswa kwa watoto wanaolazwa kwenye vitanda vya wazazi wao mara nyingi ni rahisi kuanguka sababu vitanda havina uzio wakuwazuia kuanguka tofauti na kitanda cha mtoto kinakuwa na usalama  zaidi sababu ya king’o  za kitanda kumzuia kuanguka.

Nini mzazi unatakiwa uzingatie iwapo  mtoto ameanguka

Wazazi wengi wanapata mshtuko pale wanaposikia mtoto kaanguka. Anapoanguka toka kwenye kitandani,sofa,au ngazi huwa wanatoa vilio vikali au kawaida .Kilio chake kinaweza ashiria kaumia kiasi gani au laa. Kama akipayuka sana ujue huyu ameumia kuliko maelezo, ila kuna wengine wakianguka anachukua dakika kadhaa kuanza kulia.

Ni vizuri kumchunguza haswa pale alipoangukia kama kuna uvimbe ,kavunjika au laa kwa kumpapasa lile eneo  taratibu kama atalia au kusikia maumivu  ili iwe rahisi kujua kama amepatwa na tatizo lolote.

Iwapo imetokea  mtoto ameanguka na kaangukia kichwa hiyo huwa ni hatari  zaidi na kama alianguka kwa kasi sana hapo we muwahishe hospitali kwa uangalizi zaidi ,sababu anaweza kuwa amepata kuvuja damu kwa ndani au mdhara mengine yoyote yasio onekana kwa macho mpaka vipimo hospital.

.

Hizi ni baadhi ya dalili hatari zinaweza onekana kwa mtoto baada ya kuanguka unatakiwa uwahi hospital

Mtoto anapoanguka kuna majeraha ya kuonekana kwa mara moja utaona kama uvimbe,kuchubuka,kupasuka n.k , Ila kuna mengine yanachukua muda kujitokeza na yanakuja na  dalili nyingi tofauti baada ya masaa machache au masaa 24 kama

 • Kushindwa kupumua
 • Kushindwa kuongea,kuona vizuri
 • Anatapika zaidi ya mara tatu
 • Anapoteza balance yake ( anapepesuka yaani kukaa hawezi  au kusimama)
 • Mtoto anakua sio wa kawaida kama jana au juzi, anachelewa kukuelewa vizuri anakua kama amezubaa flan hivi (motor skills)
 •  Mtoto anapata shida kulala au kuamka, yaaani akilala kumuamsha inakua ni shida mpaka amshwe sana.
 • Macho kubadili mwelekeo (iyo inaweza kuwa amejionga kibaya kichwani na kuapata majeraha ndani  ya ubongo.
 • Kulia mara kwa  mara au kupiga kelele kwa sauti kali(screaming)

Njia za kumwepusha mtoto asiweze kuanguka

Ningumu kusema moja kwa moja unaweza kuzuia kuanguka kwa mtoto mana wanakuwa na pilika nyingi za michezo.Ila unaweza kuzuia kwa kiasi flani ili asianguke na kuumia viabaya iwapo hutokuwa karibu yake.

 • Unaweza mzungushia mito pale alipokaa kama ni mtoto mdogo

Vizuri alale kwenye kitanda chake ni kuna usalama zaidi , iwapo atalala kitanda cha wakubwa jaribu mzungushia mito au unaweza nunua uzio wa kitanda huwa inauzwa maduka ya watoto.

 

 • Epuka kuweka viti virefu ,meza,stuli n.k ili kuepuka asipande juu
 • Epuka kuacha madirisha wazi kama kuna sehemu ya yeye kuweza kupanda.
 • Epuka kumwacha mtoto peke yake , ni kheri umweke kwenye baby walker kuliko kumwacha chini au kitandani peke yake.
 • Kama unaishi nyumba yenye ngazi kwa ndani kuna vigeti(rails) vinauwa maduka ya watoto vinasaidia mtoto asiweze kushuka chini ya ngazi na kuanguka
 • Epuka kuweka vitu vingi chumba cha mtoto vinavyoweza mwangukia
 • Kitanda cha mtoto kichushe kiwe chini kabsa zile chaga zake ili ashindwe kupanda juu nakutaka kutoka mwenyewe

 

Kama mtoto wako  alishawahi kuanguka  basi hauko peke yako maana hapo chini ni baadhi ya kesi za kina mama ambao walikutwa na mkasa huu

“Nilikua na hofu sana kipindi mtoto wangu wa miei 6 alipoanguka kitandani. Nilimuacha amelala kitandani na nilimuwekea mito imemzunguka alafu gafla nikasikia Bloog! af kikafatia kilio kikubwa. Nilimwangalia kwa kamsaa 24. Ahsante mungu kwa sababu aliendelea kuwa ama kawaida alikuwa kawaida tu kama vile hamna kitu kilichotokea. Nahisi malaika wake walimlinda asiumie”

 

“Nilikua namnyonyesha mtoto wangu wa miezi 4 kitandania alafu tukapitiwa na usingizi. Mara nikasikia mtoto analia niliangalia nikakuta mtoto wangu ameanguka chini na kujigonga kichwa. Ninahofia labda anaweza kuwa anavuja damu kichwani. Nifanyeje”.

 

” Daktari wangu aliniambia nimwangalie mtoto kama analaaaaaa tu bila kuamka au anatapika sana, kama sio na kama anaendelea kuonekena yuko vizuri na yuko kawaida kama basi hamna haja ya kupanic.

Mtoto wangu wa kiume wa miezi 9 ameanguka kwenye kitanda kwa mara ya pili sasa na bado sielewi kwa nini. Baada ya dakika 5 za kulia na kisikilizia maumivu amesharudi kuchezea midoli yake. Malaika wa mbiguni walimlinda”