Maziwa Ya Ng’ombe Kwa Mtoto

Wakina mama wengi huwa wanaanza kwanza kumnyonyesha mtoto kitu ambacho ni sahihi kabisa maana unashauriwa miezi sita ya mwanzo ni lazima kumnyonyesha mtoto wako.

Sasa kwa upande wa maziwa ya ng’ombe hasa inashauriwa mtoto akifikisha miezi 12 ndio inakua vizuri kuanza kumpa maziwa hayo. Mfumo wa chakula wa watoto wadogo huwa hawawezi kumeng’enya maziwa ya ng’ombe kuliko ya mama akiwa bado ni mdogo hasa chini ya mwaka mmoja kwa sababu maziwa ya ng’ombe yana protein nyingi sana ambayo yanaweza kuharibu mfumo mzima wa chakula mwilini mwake.

Maziwa ya ng’ombe hayana madini ya kutosha na vitamini C na vitamini zingine za mtoto mchanga kwa hiyo zinakua sio nzuri kwa watoto wachanga na kama akinywa wakati bado umri ni chini ya mwaka mmoja anaweza kupata matatizo kwenye mfumo wa chakula.

 

Kwanini Mtoto Wako Anatakiwa Kuanza Kunywa Maziwa ya ng’ombe.

Maziwa ya ng’ombe yana vitamini aina ya Calciaum ambayo vitamini hizi ni nzuri kwa ajili ya mifupa na meno vile vile huwa inasaidia mzunguko wa damu kuwa mzuri na mishipa kuwa katika mahala pake kwa hiyo yana saidia sana. Faida nyingine ni kwamba maziwa ya ng’ombe yana vitamini D anayosaidia ukuaji wa mtoto kuwa mzuri na wa kawaida na kufanya vitamini zingine kama calcium kufanya kazi zake vizuri na kumpa mtoto wako nguvu ambazo anahitaji kwa siku nzima, na kitu kingine ni kwamba mtoto wako akiweza kupata calcium za kutosha anaweza kuondokewa na tatizo la kuwa na presh ya damu.

Je ni lazima kuacha kumnyonyesha maziwa yangu baada ya kuanza kumpa maziwa ya ng’ombe?

Wala hamna tabu kuacha kumnyonyesha na sio lazima kuacha. Unaweza kuendelea kumnyonyesha kama kawaida ilimradi wote wewe na mtoto wako mnafurahia kuendelea, hamna tabu hasa kwa watoto ambao wamefikisha mwaka mmoja. ┬áNjia nzuri ya kuanza kumpa mtoto maziwa ya ng’ombe ni kwa kuanza kumchanganyia ya kwako na ya ng’ombe kidogo maana watoto wengine wanaweza kuwa wabishi kunywa maziwa ya ng’ombe so pengine unaweza kuchanganya uone kama ataweza kunywa.

 

Ni Kiasi Gani cha Maziwa Unaweza Kumpa Mtoto?

Kwa watoto ambao wamefikisha mwaka mmoja ni vema kumpa kikombe kimoja au kimoja na nusu cha maziwa ya ng’ombe, ila kama mtoto amefikisha miaka miwili unaweza kumpa vikombe viwili 2 vya maziwa ya ng’ombe.

Ila sasa usimpe mtoto vikombe vinne 4 kwa siku ukifanya hivyo anaweza kukosa sehemu ya kuweka chakula maana tumbo utakua umelijaza maziwa na mtoto atahitaji kula pia. Kama ataonekana bado ana kiu mpe maji yatamfaa.

 

Je Kama Mtoto Wako Hataki Maziwa ya Ng’ombe Utafanyaje?

Kuna baadhi ya watoto ni wasitaarabu wanapopewa maziwa ya ng’ombe wanakubali haraka na wanaendelea kama kawaida, ila sasa kuna wale wenzangu na mie yaani wanataka maziwa ya mama mda wote. Kitu ambacho unashauriwa kuanza kufanya baada ya kugundua hilo ni kumchanganyia maziwa yako ya mama na ya ng’ombe kisha umpe. Mara nyingi huwa inasaidia kidogo kwa yeye kuanza kuyazoea maziwa taratibu, na ratibu uwe unaongeza mchanganyiko wa maziwa ya ng’ombe mpaka wakati atakapokuwa anakunywa maziwa ya ng’ombe 100%