Maswali 7 Ya Kujiuliza Kuhusu Mtoto Kwenye Week Yake ya Kwanza

mtoto wa wiki moja

Kupata mtoto na kumleta nyumbani huwa inaleta furaha katika familia hasa kwa mama na baba. Sasa kama ni mara yako ya kwanza haijalishi umejiandaaje ila bado jiandae kuwa surprised na mtoto wako na kujifunza mambo mengi kutoka kwake na maisha yake kwa ujumla.

Wakati unaanza maisha mapya na kichanga chako basi ehm angalia vitu ambayo unatakiwa kuvijua na ambavyo vinaweza kutokea kwenye week ya kwanza baada ya kujifugua.

 1. Jinsi Gani Nitatengeneza Mahusiano na Upendo na Mwanangu?

 

Kutengeneza mahusiano na upendo na mwanao ni kitu cha furaha sana  hasa ukigundua kuwa tayari ameshagundua kuwa wewe ndio mama yake. Umeshawahi kumbeba mtoto alafu akaanza kulia kwa nguuvu ila ukimrudisha kwa mama yake anaacha kulia mara moja. Sasa huo ndio upendo wenyewe. Ila kwa hali ya kawaida kutengeneza huu ukaribu wa mama na mwana huwa hauji mara moja tu huwa kuna vitu wewe kama mama unatakiwa kuvifanya ili  utengeneze ukaribu na mtoto wako

 

 • Tumia mda mwingi kuwa nae; mbebe mtoto wako vizuri karibu na kifua chako wakati unamnyonyesha au wakati unambembeleza. Unaweza pia kuwa unampa massage kwa mbaali taratibu
 • Ongea nae. Yes ongea na mtoto wako , huwa wanapenda kusikia sauti yako na unamfundisha aizoee sauti yako, ongea nae muimbie, mpaka atakuelewa.
 • Muangalie kwenye macho yake na umchekee: ukiendelea kufanya hivyo utanaona baada ya mda anakuigiliza jinsi unavyo fanya.

 

 1. Mara ngapi Mtoto Wangu Atakuwa Analala?

Mara Nyingi, kwa kipindi cha mwanzoni anaweza kulala hadi kwa masaa 16 kwa siku.  Ila sio yote mfululizo. Watoto wadogo huwa wanalala kwa saa 1 mpaka 2 ndio anaamka alafu tena atalaa kwa masaa hayo hayo…hawezo kulala masaa 3 au manne mfululizo, ni saa moja au mawili kasha ataamka. Style yao ya kuamka wote tunaijua,  ni atalia weee mpaka uje kumyanyua.

 

Jaribu Kufanya Hivi Kumsaidia Mtoto Wako Kulala Vizuri

 

 • Kama akishituka usiku na kuanza kulia, tulia kwanza kwa dakika mbili uone kama atarudi kulala mwenyewe, usikimbilie kumbeba ndio ataamka kabisa.
 • Kuwa kimya nyakati za usiku wakati unamnyonyesha au wakati unambadilisha nepi. Jaribu kuwa mtulivu usimuamshe mara kwa mara.
 • Uwe mchangamfu wakati wa mchana ili awe na yeye acheze cheze tu ili ikifika usiku alale vizuri kwa kuchoka.

 

 1. Mara Ngapi Mtoto Anatakiwa Kunyonya na Ntajuaje kama Ameshiba?

 

Mtoto anatakiwa kunyonya kila baada ya masaa 1 au 2. Utajua mtoto ameshiba  kama

 • Anatumia dakika kuanzia 10 kwa kila ziwa unapoanza kumpa kunyonya
 • Kama unambadilisha nepi kuanzia mara 6 na kutoa haja kubwa kila baada ya masaa 24 kuanzia siku ya nne.
 • Baada ya kupungua uzito week ya kwanza basi ataanza kuongezeka uzito week ya pili, kama unafatilia uzito wake basi ukienda hospitali muangalie uzito kama umeongezeka.

 

 1. Mara Ngapi Natakiwa Kumuogesha Mtoto Wangu Mchanga?

Mtoto unatakiwa kumuogesha mara 4 ndani ya week  au mara tatu. Hizo siku zingine ni unampangusa tu ngozi yake kwa sababu bado ni mdogo sana kumuogesha kila siku vile vile unatakiwa kusubiri mpaka kitovu chake kikauke. Kama unaona kuna uhitaji wa kutumia maji basi usimwagie tumia kwa kupangusa sio kumwagia.

mtoto wa wiki moja

 1. Nitafanyaje Kumlinda Mtoto Wangu Kutoungua Kutokana na Haja Kubwa?

Njia ni moja tu. Hakikisha unamtunza mtoto wako katika hali ya usafi mda wote. Hiyo inamaanisha ukigundua kuwa ameshafanya biashara zake bila kukwambia basi unatakiwa kubadilisha nepi mara moja ili asiungue na mkojo au haja kubwa maana kadri anavyokaa na  uchafu kwa mda mrefu ndio unaungua.

 

Watoto wadogo wana ngozi laini sana, kwa hiyo unatakiwa kumsafisha kila sehemu na taratibu, tumia maji ya moto na kitambaa laini baada ya hapo mpanguse na taulo laoni iliyokauka. Usimpanguse kwa nguvu.

 

 1. Jinsi Gani Natakiwa Kukitunza Kitovu cha Mtoto Wangu.

Wakati mtoto amezaliwa kitovu chake huwa bado hakiko sawa kwa hiyo wakati huo unatakiwa ukitunze na kuhakikisha kuwa eneo lote la kitovu panakaa pakavu mpaka kitakapo pona kabisa.

 

Msafishe mtoto wako kwa kutumia sponge au nguo laini na usiweke maji kabisa kwenye kitovu na nepi unavyo mvalisha hakikisha

 

Kama ukigusa kitovu alafu mtoto wako akawa analia basi mpeleke kwa dakitari kutakuwa na maambukizi flan ameyapata.

 

 1. Kitu Gani Kingine Natakiwa Kufanya?

Enjoy na ufurahie kuwa na mtoto wako mchanga na uendelee kujifunza vitu vingi kutoka kwake maana hawa nao wanakuja na vitabia  vya kila aina. Kumbuka

 • Kila mara mlaze mtoto wako kimgongo mgongo
 • Toa kila kitu kwenye eneo lake la kulala ili kuwe na hewa nzuri inayo mzunguka, usiweke mto, wala midori
 • Mtoto wako anatakiwa kulala chumbani kwako, sio unamuweka chumba kingine na wewe chumba kingine.
 • Hakikisha unafata ushauri wa daktari na kuuzuria vipimo kila mara unapoona hali si shwari.
 • Mnyonyeshe mtoto wako kwa wakati
 • Mvalishe mtoto wako simple tu. Usimjazie jazie manguo ya kila aina.