Mara Ngapi Mtoto Anatakiwa kupata Haja Ndogo

Kina mama wengi huwa wanauliza hili swali ni mara ngapi mtoto anapata haja ndogo, na hii hutokea pale wanapogundua kuwa mtoto hapati haja ndogo kwa mda flan. Sasa katika hali ya kawaida ni vigumu kujua ni mara ngapi mtoto anatakiwa kutoa haja ndogo na hii inatokana na sababu mbali mbali kama umri, na mtoto mwenyewe alivyo. Hapa kuna baadhi ya mambo nimekuwekea unaweza kuangalia ili kujua mtoto wako yukoje

 

  • Kwa watoto wadogo kabisa kwa kawaida wanatakiwa kutoa haja ndogo mara 6-8 ndani ya masaa  24 pamoja na haja kubwa mara baada ya siku kadhaa baada ya kuzaliwa. Kwa sababu utumbo wa mtoto unakua ni mdogo kwa hiyo atakua anatoa haja ndogo na kubwa mara nyingi ndani ya siku. Zile siku za mwanzo kabisa baada ya kuzaliwa mtoto anaweza asitoe haja ndogo kabisa, kwa watoto ambao wana masaa 1-5 tangu wazaliwe wakitoa haja ndogo nikawaida so usije kushangaa.
  • Kwa watoto wakubwa kwa sababu utumbo wao ni mkubwa na wameanza kula vyakula vigumu kwa hiyo unakuta kutoa haja ndogo inakua mara chache sana.
  • Kuna wakati mtoto wako anapokua anaweza kuanza kuweza kucontrol haja ndogo na asiende uani mara tu baada ya kusikia amebanwa. Mtoto anaweza kuubaana kwa mda flan kwa hiyo ukisema mbona haendi kila mara kumbe mwenzio kajibana bana wala hana tatizo lolote.
  • Kwenye mazingira ambayo ni joto sana mtoto anaweza kutoa haja ndogo mara chache kama watu wazima.
  • Kwa upande wa haja kubwa mtoto wa kuanzia mwezi mmoja na miezi miwili anaweza kukaa hata siku mbili hajatoa haja kubwa na hii huwa ni kawaida. Ila kuna baadhi ya watoto wanaweza kuwa hivi na wengine wasiwe hivi cha muhimu wewe kama mzazi ni kumchunguza mtoto wako na kumuangalia kama kweli afya yake ni nzuri na kumlisha chakula kizuri na maziwa kumnyonyesha kwa wakati. Watoto wanazaliwa tofauti.

 

Kwa masaa 3 kama mtoto wako hatoi haja ndogo hii ni kawaida kabisa na inategemea na umri wa mtoto wako na afya yake kwa ujumla.

Kama mkojo wa mtoto wako hauna harufu kali na hauna rangi ya  njano basi mtoto wako yuko vizuri. Kuna baadhi ya dalili za ugonjwa, kama mtoto hali chakula vizuri au kunywa maji ya kutosha, au anasikia maumivu kwa hiyo ni vema kuwa unamchunguza mara kwa mara.

 

Kuna wakati mwingine kama mtoto wako ni mchanga anatoa haja ndogo kila mara na ni mara nyingi kuliko kawaida pengine hii inaweza kuwa ana matatizo kwa hiyo inabidi umpeleke hospitali.