Mama Baada Ya Kujifungua

Baada ya mama kujifungua mtoto kuna mambo mengi yanakuwa yanabadilika kwenye maisha yake ukilinganisha na zamani. Mfumo wa maisha yako unabadilika kwa kiasi kikubwa mfano muda wa kulala na kuamka, ulaji wako unaongezeka zaidi.

Lishe

Kwenye hayo mabadiliko yapo pia ya mwili, kwa kiasi kikubwa wamama wengi baada ya kujifungua wanawazia miili yao kuongezeka uzito. Nikweli mama anaweza ongezeka uzito haswa kipindi cha miezi  2-3 baada ya kujifungua. Hutakiwi kujistress sana sababu ya unene ukakosa kula vizuri na kuzalishe maziwa ya kutosha kwa mtoto.

Unachotakiwa kula mlo kamili wenye virutubisho vya kutosha kama wanga, mafuta kidogo, protein,n.k. Vyakula vya  kula mama alitoka kujifungua ni vingi ila jitahidi kula vyakula vyepesi na maji maji (soup) kwa siku 40 za mwanzo.

Mazoezi

Mama anahitajika kufanya mazoezi. utaanza kwa mazoezi mepesi kama kutembea, kuruka kamba wiki 3-4 baada ya kujifungu. Kwa mazoezi mazito kama ya gym ni vizuri ukasubiri kwa muda wa wiki 6-8 , hapo mwili utakuwa umesharudisha nguvu.

Tamaduni za mabibi zetu walikuwa wakifunga khanga tumboni badaa ya kujifungua ili kusaidia tumbo kurudi kwenye hali yake ya kawaida.

Njia Rahisi Za Kupunguza Tumbo

  • Kuangalia chakula unachokula -kisiwe na mafuta mengi au wanga mwingi (wali /ugali/chapati)
  • Kunywa supu  inasaidia tumbo kupunga kwa urahisi
  • Kula mapema chakula cha usiku
  • Ukifunga khanga / corset yako hakikisha unaivaa kwa masaa sio chini ya masaa 6 kwa siku

Sema Ndio Kama kuna mtu anataka kukusaidia.

Huu ndio mda mzuri wa kusema ndio kama kuna mtu anataka kukusadia kwa sababu ni kweli unakuwa unajisikia vibaya wakati mwingine na usione aibu kusema nisaidie kitu flan. Wakati mwingine ukishajifungua watu watu majirani marafiki huwa wanataka kuja kukuona, vile vile sema hapana kama umeona wageni wamezidi.

Kuwa Makini unapojisikia uko mpweke.

Kuna wakati mwingine kwa kuwa umetoka kujifungua unakuta wamekuacha hapo sebuleni au chumbani umepumzika. Gafla unajikuta uko mpweke na kama vile watu ndani wamekususa. Nooo ukisikia hali kama hii ni vema ukaongea na watu waliopo ndani wawe wanakuja kukuangali mara kwa mara au ongea na rafiki zako wawe wanakupigia simu atleast kukujulia hali, hii itakufanya usijisikie mpweke maana watakuwa wanajua hali yako.