Maandalizi Ya Mama Mjamzito Kwa Ajili Ya Mtoto

Anapenda Kubebwa Mda Wote

Maandalizi ya mama mjamzito kwa ajili ya mtoto ni muhimu kabla hajajifungua na baada ya kujifungua. Mama anaweza kuanza fanya shopping baada ya kufanyiwa Ultra sound kujua jinsia ya mtoto, ili kuepuka gharama ya kununua nguo mara mbili iwapo kama utakosea jinsia ya mtoto.

Mimba ifikapo miezi 6-7 hapo mama anaweza anza kununua mahitaji ya mtoto na hapo chini tumekuwekea list ya vitu unavyoona vitakufaa

 • Nguo-ukinunua nguo za mtoto usinunue size ndogo sana , kwa sababu watoto wachanga wanakuwa haraka mno.
 • Kofia-mnunulie 2-3 ni muhimu mtoto mchanga kufunikwa kichwa.
 • Masweta-nunua 2 yatamsaidia jioni kukiwa na kibaridi.
 • Taulo-1.
 • Soksi-nunua pair 3 au zaidi.
 • Beseni la kuogea-1
 • Sabuni au shampoo ya mtoto isio na harufu kali.
 • Sanduku au kabati la kuhifadhia nguo zake.
 • Nepi au diapers-utanunua nepi pair 12 au zaidi ukiweza ,ili iwe rahisi
 • Mtoto kubadilishwa nepi mda wowote iwapo zimechafuka.
 • Neti kuepuka mmbu- Malaria ni hatari kwa watoto usimlaze bila kutumia neti.
 • Bibs- kama kaapron ivi utamfungia shingoni akicheuwa au udenda ukimtoka hautomlewesha.
 • Cotton buds- kusafishia masikio .
 • Mafuta ya nazi – watoto wachanga wanakuwa na ngozi kavu ,mafuta ya nazi yanawafaa zaidi.
 • Wipes au vitaulo vidogo -utatumia kumfutia akjisaidia au kumfutia baada ya kumnawisha na maji safi.
 • Kitana.
 • Nail care-utatumia kumkatia kucha ili mtoto asijikwangue usoni.
 • Khanga au vitenge- mama atatumia kumbebea au kumfunika.
 • Kitanda cha mtoto kwa watakao weza – kina mfanya alale kwa usalama zaidi tofauti na kitanda cha watu wazima ni rahisi kuanguka akijigeuza.
 • Mashuka 2-3 ya kutandikia na kumfunikia.
 • Kiti chake cha kumkalisha kwenye gari- kwa wenye magari epuka beba mtoto bila kiti chake na kumfunga mikanda itamwepusha  kurushwa nje ya gari au kujigonga vibaya iwapo itatokea ajali.
 • Stroller-ni kigari anachokaa na kusukumwa mtoto ila iwapo mzazi utapenda ndio utanunua,na ukimkalisha hakikisha umemfunga mikanda ili asianguke.