List Ya Vitu Asivyotakiwa Kula Mtoto Chini Ya Mwaka 1

Watoto wachanga  wana miili isiyo komaa bado wanakuwa wanahitaji kulelewa kwa umakini na kwa kuzingatia lishe .Mwili wa mtoto alie chini ya mwaka hauna kinga ya kutosha kupigana na bacteria au virus wanao tokana na vyakula .Hivyo mzazi inakubidi kuwa makini kwa kupika kwa kuzingatia usafi na kuosha matunda na mikono yake kabla ajala.

unnamed (3)

 

 

Hii ni list ya vitu asivyotakiwa lishwa mtoto mpaka atakapo fikisha mwaka 1

 

 • Asali -kaiwa inatabia ya kubeba bacteria ambao wanakuja kumwadhiri mtoto japo hao bacteria kwa mtoto wa mwaka 1 mwili wake unakinga ya kupigana nao,ila kwa alie chini ya mwaka 1(miezi 12) si rahisi hivyo ni vizuri asipewe.

 

 • Mafuta ya kupikia -mtoto haitaji mafuta kwenye chakula chake kwani vyakula anavyopikiwa vinamafuta ya asilia kama nyama,kuku,samaki iwapo ukatumia mafuta tumia butter isiyo na chumvi  au Olive oil ni mazuri hayana calories kama mafuta mengine na  na yatamsaidia kwenye ukuaji wa ubongo wake.

image

 

 

 

 • Soya-inatengeneza allergy ,inapoteza vitamins,minerals ,amino acid na fatty acid kwenye mwili wa mtoto hivyo ni vizuri wapewe wakiwa na umri zaidi ya mwaka 1.

 • Chumvi -wazazi wengi wanadhani chakula kisipo na chumvi mtoto hawezi kula hapana yeye ndio anaanza jifunza kula hajui ladha yoyote kuwe na chumvi au lah ,chumvi ina madini ya sodium ambayo yanaweza kwenda kuadhiri figo au  ikaenda hadhiri moyo na kupata matatizo ya  (high blood pressure) hivyo haitajiki chakula kiwe na chumvi hata kama ikatumia ni kiwango kidogo pima kwa vidole kidogo sana.

 

image

 

 • Sukari -kiwango kikubwa cha sukari sio kizuri kwa watoto inamwaribu  meno ya mtoto ,ufisi upo kwenye process za kuoteshwa meno iwapo mtoto akapewa sukari hapo anaharibu ukuwaji wa meno , au mtoto kupata matatizo ya kisukari baadae. Kwenye uji unaweza kutumia ndizi mbivu inasukari ya kutosha kwa kutumia kwa chakula cha mtoto,saga ndizi mbivu then changanyia kwenye uji  ulio shaiva utapata sukari asilia na ladha nzuri ,ukishindwa tumia kiwango kidogo sana cha sukari.

image

 

 

 

 • Maziwa ya ngo’mbe-haya yana madhara zaidi japo jamii yetu ya Tanzania iashazoea vizazi na vizazi wanapewa maziwa ya ngo’mbe ila kiukweli ni makosa yana protein nyingi sana ambayo mtoto hawezi kuimudu kuisaga na inakuja kusababisha madhara kwenye Ini baada ya mda mrefu,pili yana leta allergies kwa watoto unaweza mpa mtoto maziwa ukaona anatapika au kuhara hapo usimpe mwache ,ukiendelea kumpa itatengeneza allegry na baadae atashindwa kutumia dairy product yoyote ,Tatu ng’ombe akipewa madawa akiwa mgonjwa au chanjo yanakimbilia kwenye maziwa na ndio hayo mtoto anapewa itakuja kuwa sumu mwilini mwake na kumwadhiri.

image

 • Vyakula vibichi -vinaweza mpa bacteria kama mayai mabichi,nyama au samaki (sushi)

 

 • Saturated fat-vyakula vyenye mafuta kwaa wingi chips,crips,burger au cakes mtoto asipewe,hata chocolate ,mabisi au ice cream asipiwe umri wake bado.

 

 • Samaki wa wenye madini ya zebaki(mercury)nyingi  kama papa ,chuchunge,dagaa wakubwa n.k wataadhiri nervous system,badala yake mpe sangara ,sato au salmon wana hawana mercury nyingi hawa wana mafuta ya kutosha na omega 3 zitakazo msaidia kukuza ubongo na kumfanya kuwa na akili.

image
SAMAKI WENYE ZEBAKI ( MERCURY)NYINGI
 • Nuts-karanga au korosho mtoto asipewe kutafuna itamkwama kooni kama ni karanga basi iwe ni yakusagwa  na wapewe watoto kuanzia miezi 6 ila fahamu karanga zinaleta allergy kwa baadhi ya watoto.

 

 

 

Ushauri 

 

 • Hili swala la maziwa ya ng’ombe ni hatari kwa watoto,ingawa watu wengi wanapenda kulipinga kwa vile tumeona jamii yetu inakuza watoto kwa kutumia maziwa ya ng’ombe tangu miaka iyo ya mababu zetu,kukumbuka nchi yetu haina taratibu ya kufanya tafiti  mara kwa mara kama kwenye nchi za kuendelea huwezi shauriwa na mkunga au daktari umpe maziwa ya ng’ombe mtoto alie chini ya mwaka 1 wanajua madhara yake na wanatafiti nyingi juu ya hilo,ni umaskini wetu Africa wa kushindwa kuaafford baby formula (maziwa ya kopo) ndio unatufanya tuwape watoto haya maziwa,mwisho nakushauri ongea na daktari  mzuri wa watoto atakwambia ukweli  kama huu huu juu ya maziwa ya ng’ombe kabla ujampa mtoto.