Jinsi ya kulea mtoto ukiwa Peke Yako (Single Parent)

kulea mtoto ukiwa single parent

Kabla ya kuwa na mtoto watu wengi huwa na picha ya kuwa na familia ni ya wazazi wawili. Ila katika hali ya kiuhalisia mambo huwa ni tofauti na unakuta mtu anabakia kuwa peke yake tu na mwezie anakua hayupo kwa sababu mbali mbali ambazo zilipelekea wakaachana. Japokuwa kama utakua hujui, kulea mtoto ukiwa peke yako huwa ni kazi kubwa na wakati mwingine unaweza kuwa na furaha na kuenjoy. So hapa nataka nikupe tips na njia ambazo unaweza kuzitumia ili uweze kumlea mtoto wako wakati upo single na kumuweka mtoto wako katika mazingira ya kawaida tu.

Tafta Msaada

Unaweza kuwa unamlea mtoto wako mwenyewe ila hauko peke yako. Lazima utakua na ndugu au marafiki ambao wako tayari kukusaidia kwa namna moja au nyingine basi waruhusu wakusaidie. Kama huna ndugu wa kukusaidia au marafiki wanasema wako busy na mambo yao basi tafta msaada kwa watu wengine kama kuna watu unajua nao wanalea watoto wao peke yao basi anzisha urafiki

nao ili muweze kubadilishana mawazo. Kitu ambacho unatakiwa kujua ni kwamba kuanzisha mahusiano na mtu mwingine ni rahisi hasa katika nchi yetu hii yenye amani mda wote.

Balance mda wako na kazi

Maisha ya mzazi ambaye analea mtoto wake peke yake yako busy. Ukiachana na kazi za kulea mtoto kumuogesha, kumlisha mara umbembeleze, bado unakazi za ofisini na boss wako nae mkali kuliko  hata mama yako. Kwa hiyo ni muhimu kupanga jinsi unavyoweza kupangilia mda wako ili usichoke sana na uendelee kuenjoy maisha.

  • Kubali kusaidiwa. Kuna wakati majirani ndugu au marafiki wanaweza kuja nyumbani kukusalimia na wakataka kukusaidia waruhusu wakusaidie.
  • Jifunze jinsi ya kulea mtoto vizuri. Kuna wakati mzazi ukiwa peke yako inakua ngumu kujua vitu mbali mbali kwa hiyo chukua mda kujifunza mambo mbali mbali kuhusu kulea watoto. Tumia maeneo ya watoto ambayo yamepangwa kuchezea mpeleke mtoto wako afurahie kama ni shuleni kwao basi ukienda kumchukua mpe mda wa kucheza kidogo.
  • Kama huna mda wa kuwa na mtoto wako jaribu kuangalia kama unaweza kupata mda. Kwa mfano angalia kama unaweza kuwahi nyumbani, zingatia mda ili uwe na mda mwingi na mtoto wako.
  • Usisahau kufurahia maisha. Chukua break na urelax. Mara nyingi kama uko peke yako unaweza kusema huna mda wa kutulia na kurelax. Ila ukweli ni kwamba mda upo kama ukiupangilia vizuri hasa kama una mtoto mmoja tu au wawili. Kwa mfano Hizi weekends jamani zina maana kubwa. NI WEEKENDS JUMAMOSI NA JUMAPILI………. ni siku za kupumzika hiyo inajulikana dunia nzima kwa hiyo unaweza kabisa kuamua kuzitumia hizi weekends kama zinavyotakiwa  kutumiwa. Ikifika weekends tulia na relax.
  • Jipe mda. Kujipa mda ni muhimu na ni kitu rahisi. Kama mtoto wako amelala, na wee unaweza kulala kidogo, chukua hata 30 za kupumzika au 15.

jinsi ya kulea mtoto ukiwa peke yako

Onyesha Mfano.

Watoto wanafurahia wakijifunza kwa wazazi ambao wanawaonyesha mambo mazuri. Muonyeshe mtoto wako matendo mazuri, tafuta ndugu zako na waambie marafiki zako wawe na tabia nzuri na kama ukiona kuna watu ambao unaona wana tabia za ajabu ajabu

basi hakikisha hawatakaa na mtoto wako kwa mda mrefu maana wakikaa nae kwa mda mrefu kama unavyojua lazima atajifunza tu mambo mengine ambayo hatakiwi kujifunza. Kwa hiyo angalia watu wanaokaa na mtoto wako wawe na tabia nzuri.

Kama Ukizidiwa.

Kuwa na mzazi ni kazi ngumu na hasa kama uko peke yako ndio balaa kabisa. Kila mzazi kuna mda huwa wanakua na hasira wananuna na kukasirika. Sasa jamani please usimalize hasira zako kwa mtoto na kumnyima chakula au kuacha kumnyonyesha kisa umenuna!!!!!. Ndio nakwambia sasa kama ukiwa na hasira au kuna mtu kakuudhi huko basi ukiwa mbele ya mtoto wako mchekee kama vile hamna kitu kinachoendelea. Ukihamisha hasira zako kwa mtoto utakua unamuumiza na yeye alafu huwezi jua unaweza kuishia kwenda hospitali kwa sababu ya hasira zako. Wapo watu wengi wanajikujikuta wanaenda hospital kwa sababu ya hasira au kuwa ameuthika na mtu flan so angalia usije kuwa ni wewe.