Kukoroma Kwa Mtoto Akiwa Amelala

kuna sababu  tofauti zinazompelekea mtoto kukoroma kipindi akiwa amelala ,zinaweza kuwa tatizo la kiafya au mabadiliko ya mwili. Mzazi anaweza kujua upumuaji na ukoromaji wa mtoto sio wa kawaida kwa kumfatilia kiumakini. Tatizo la kukoroma  lipo kwa watoto wengi na hutibika kinachotakiwa mzazi kumpeleka mtoto kituo cha afya kwa vipimo zaidi.

 

CHANZO CHA KUKOROMA

:Mafua-mtoto anakuwa na mafua au kifua anabanwa sana kushindwa kupumua vizuri na kumsababishi kukoroma

:Uzito mkubwa wa mtoto (unene)

:Mafindo findo (tonsils and Adenoid) hizi zinatengeneza kitu kama uvimbe kwenye koo na kumfanya akorome sana.

ADENOID

Adenoid ni tissue ambazo kila binadamu anakuwa kazaliwa nazo zinapatikana kwenye nasal  cavity. Mtu anavyokuwa kiumri nayo yanasinyaa, iwapo mtu akapata bakteria au virus basi zitamshambua na kumpa uvimbe kwenye koo ,uvimbe huo unatengeneza maji maji mengi yenye uterezi (mucus).

 

PICHA IKIONYESHA UVIMBE KINYWANI

 

:Obstrutive sleep Apne- ni aina nyingine ya Adenoids inayo msababishia mtoto kushindwa kupumua na kubanwa  pumzi pale hewa inapoingia na kutoka,hali inayo inamfanya mtu asilale vizuri amke kila mara kwa mshtuko pale mapafu yanaposa hewa.

:Infection ya masikio-(otitis) adenoid inaenda kuziba mishipa ya ya sikio na kusababishia infection.

TIBA

Unapoona mtoto anakoroma na hana mafua wala kifua ,basi usizembee mpeleke hospital atafanyiwa vipimo vya :ACT, X-RAY, au MRI

Adenoids inapokuwa imevimba sana na kuwa kubwa basi itabidi ipasuliwe,na  iwapo sio kubwa na ikawa imeletwa na bakteria tu basi utandikiwa antibiotics.Hili tatizo linawapata watoto na watu wazima pia.

MATHARA YANAYOLETWA NA ADENOIDS

.Matatizo ya moyo

:High blood pressure

.Kisukari

Kiharusi(stroke) kupooza mwili.