Je Mwili Wako Utarudi Kuwa Kawaida Na Kuvaa Nguo Ambazo Ulikua Unavaa Kabla Ya Ujauzito?

Sisi akina mama huwa tuna nguo zetu zileee ambazo yaani ukiwa na ujauzito unakuta nguo uliyokuwa unaipenda haikutoshi hata baada ya kujifungua bado unakua unawaza je itakua bado inakutosha au ndio kwaheri uanze kupanga mtu wa kumgawia  Jibu ni NDIO itachukua mda kidogo mpaka mwili wako urudi katika hali ya kawaida ya mwanzo.

Kumbuka kwamba  imechukua miezi tisa kumbeba mtoto tumboni mwako so huwezi kutegemea  mwili wako utarudi kama ulivyokua mwanzoni ndani ya wiki mbili au tatu au nne. Tena kama hujui inaweza kuchukua hadi mwaka mzima mwili kurudi mpaka kwenye level ambayo unaiita Kawaida, hata hivyo baada ya kurudi bado unaweza kukuta mwili umebadilika kabisa. Mfano hips unakuta zimekuwa kubwa au zimepungua, tumbo bado linakuwa kubwa, kiuno kinakua kikubwa au unanenepa tuu gafla bila mpangilio haya yote yanaweza kutokea, Kitu cha muhimu baada ya kujifungua jiangalie na kujifatilia mwili wako unabadilika vipi ili iwe rahisi kugundua mapema.

Kwa miezi ya mwanzo baada ya kujifungua unaweza kuona ni kawaida kuvaa nguo zako ambazo ulikua unazivaa wakati ulikua na ujauzito wa miezi mitano au sita au unaweza kukuta nguo ambazo zilikua zinakubana zinalegea au ambazo zilikua zinalegea sasa hivi baada ya kujifungua zinakubana.

Sasa njia nzuri ya kurudisha mwili wako vizuri na kuanza kuvaa kile kisiketi chako  ulichonunua mwaka mzima uliopita, ni kula chakula bora na kufanya mazoezi BASI! Sasa kazi inakuja kupata mda wa kufanya mazoezi ukiwa kama mama wa kitoto kichanga ni balaa, ila kitu unachotakiwa kujua ni kwamba mtoto wako ataendelea kukua na kama una msaidizi nyumbani basi ni kitu ambacho unatakiwa kutengeneza mipango ili upate mda wa mazoezi.

Yaani hapa hamna kitu kingine zaidi ya  kula chakula bora matunda vyakula vyenye kuleta vitamini mwilini na kujenga mwili na baada ya hapo fanya mazoezi kila mara. Kama unafanya kazi jumatatu mpaka ijumaa basi jipangie siku za weekend asubuhi na jioni fanya mazoezi kukimbia kuruka ruka na kila aina ya mazoezi ambayo unaweza kuyafanya, na hasa kama unaweza kwenda Gym siku hizi naona zipo nyingi  tu mjini nenda huko fanya mazoezi kikweli kweli na kama ukifanya hivi basi lazima mwili wako urudi na kuwa wa kawaida kama zamani na kuwa kama vile hujajifungua.

Good Luck.