Je Maziwa Yataacha Kutoka Kama Haunyonyeshi Mtoto Baada ya Kujifungua?

Kuna baadhi ya akina mama ambao wao hawapendi kunyonyesha watoto wao kwa sababu zao wanazozijua wenyewe japokuwa inashauriwa MIEZI SITA ya mwanzoni unashauriwa umnyonyeshe mtoto wako kama kweli unampenda kabisa. Ila Sasa je baada ya kujifungua haya maziwa huwa yanakauka au la!

Jibu ni Ndio maziwa huwa yanakauka ila itachukua mda kidogo mwili wako kuja kuanza kutulia tena.

Wakina mama wengi huwa wameumbwa hivyo tayari maziwa lazima yataanza kutoka tu, na hii hutokea tangu ukiwa na ujauzito. Ukiwa na ujauzito utagundua tu kuona maziwa yako yanaanza kuwa mazito hasa ukishafikisha ujauzito wa week 16 na kuendelea.

Unapojifungua tu mwili wako huwa unawasiliana ndani kwa ndani na maziwa yataanza kutoka kwenye matiti yako tayari kwa kunyonyesha. Hapo  uwe umepaga kunyonyesha au hujapanga matiti yako yataanza kuwa mazito  ukisha jifungua tu.

Kuna Homoni zinaitwa Prolactin. Kama hutoanza kumyonyesha mtoto wako kwa kutumia njia yoyote ile basi hizi homoni zitatuma taarifa kwenye ubongo wako na kuwa maziwa hayahitajiki na hapo basi mwili wako utaacha kutengeneza maziwa kwa ajili ya mtoto. Ila kama baada ya kujifungua na ukaanza kumyonyesha mtoto basi mwili utaendelea kutengeneza maziwa.

Maziwa

 

Kama umeamua hutaki kumyonyesha mtoto wako maziwa ya kwako mwenyewe iwe ni kwa kumyonyesha moja kwa moja au kwa kukamulia kwenye chupa basi huwa inachukua kati ya siku saba au kumi na matiti yako yanarudi katika hali ya kawaida na unakua kama vile hujawahi kujifungua kabisa.

Wakati mwingine unaweza kujikuta kuwa ukivaa sindiria unajikuta ndio inakua afadhali zaidi ila usiyabane maziwa maana ukivaa sindiria ambayo inabana sana maziwa basi utasababisha mabalaa mengine na hauta kuwa na amani wewe mwenyewe ukiyabana sana matiti so yaachie yapumue.

Kama unaona bado yanakua ni makubwa na hayawezi kukaa kwenye sindiria vizuri, basi unaweza kuyakamua na kuyapunguza kidogo ili iwe rahisi kwako kuvaa sindiria kwa urahisi. Ila kumbuka sasa ukikamua maziwa mara kwa mara kwa sababu tu ya kuyapunguza ili yakae vizuri, hapo unatuma ujumbe kwenye ubongo wako kuwa maziwa yanahitajika kwa hiyo mwili utaendelea kutengeneza maziwa kwa sababu wewe unakua unayakamua kila mara.

So kwa ushauri kama unakamua kwa ajili ya kuyaweka sawa basi kamua mara moja au mbili basi ila ukiendelea, mwili utaendelea kutoa maziwa na hiyo itachelewesha mda wa maziwa kukauka mwilini. Kitu kingine  maji ya moto nayo huwa yanaongeza kasi ya uzalishaji maziwa mwilini kwa hiyo kama upo sehemu za baridi basi hakikisha matiti usiyamwagie maji ya moto kama ni kusafisha yasafishe na maji ya baridi au uvuguvugu saaana.

I hope tumeelewana hapo. Kama unakitu cha kushare na kuongezea weka comment hapo chini….Cheers!!