Faida Za Mafuta Ya Mzaituni (Olive Oil)

bowl being poured with yellow liquid

Photo by Pixabay on Pexels.com

 Tafiti nyingi zimeonyesha olive oil (zaituni) inafaida nyingi sana Kwenye mwili wa binadamu. Badala  ya Kutumia Mafuta mengine ya  kula, tumia olive oil kwa afya yako na familia yako. Yana Cholesterol  ndogo ambayo ndio nzuri kiafya.

Spain ndio nchi inayolima zeituni  kwa wingi, unaweza ukala tunda la zeituni au ukatumia mafuta yake extra virgin oil kwa kupikia chakula, yanabei ya juu kidogo yanapatikana supermarkets kwa bei tofauti kulingana na brands bei kuanzia 10,000Tshs na kuendelea inalingana na ujazo. Mazuri kwa watoto pia wa miezi 6 na kuendelea  kupikiwa kwenye vyakula inakuza ubongo.

 Maradhi Yanayotibu au Kuepuka Kupatwa

 • Cancer-mafuta ya zeituni yana olecanthal na of mimics inayozalisha ibuprofen inayosaidia  kupunguza hatari ya kupata cancer.
 • Matatizo ya moyo
 • Blood pressure- inapunguza matatizo ya pressure ya juu na  chini.
 • Kisukari-inasaidia kucontrol blood sugar .
 • Kupunguza uzito wenye calories nyingi olive oil inasaidia kupunguza unene.
 • Hutibu maumivu  ya mifupa
 • Unajiepusha na stroke
 • Inakusaidia uwe na kumbukumbu nzuri (improve memory)
 • Zeituni inafanya moyo wako usizeeke – unavyozidi kukua moyo huzeeka
 • Inapunguza stress
 • Kukuepusha na cancer ya ngozi, vile vile cancer ya ziwa

Matumizi Yake Mengine

 • wenye ngozi kavu tumia pia massage ya watoto wachanga au wakubwa tumia (ukishikwa na misuli tumia kuchuwa)
 • Kutumia kwa urembo wa nywele husaidia kukuza nywele zilizo katika au ️ kujikunja (fungamana) unaweza changanya parachichi na mafuta ya olive oil ukapaka na  kuosha baada ya dk 20-30 ️Au ukachanganya mayai na olive oil.
 • Wenye kukosa choo watoto mchanganyie na chungwa maji kidogo na asali mpe ila asali kwa watoto wa 1yr na kuendelea .
 • Kutengenezea sabuni
 • Kutumika kama mafuta ya kupaka mwilini kukufanya kuwa nyororo na ng’avu yana vitamin A,D,E na K zinazo saidia kutoa sumu kwenye ngozi pia.
 •  infection ya sikio  kwa watoto mweke matone 2 mara 3 kwa siku.
 • Mafuta ya zaitunii yanatibu mafua unapaka nje ya tundu za pua mara 2-3 kwa siku yatakauka kwa haraka
 • Watoto na watu wazima wenye tatizo (bawasili) wameota kinyama sehemu ya kutolea haja kubwa wanapata maumivu  wakijisaidia wajipake sehemu ya aja kubwa kabla na baada ya kupata ajakubwa! Ilainishe mishipa!