Dalili Za UTI

Dalili za ugonjwa huu huwa tofauti kulingana na hatua ambayo ugonjwa umeshafikia.

U. T. I ni neno linalotamkwa kwa kifupi lakini kirefu chake ni, “Urinary Tract Infection” likimaanisha, “Maambukizi katika njia ya Mkojo. ”

Kitu kibaya zaidi ugonjwa huu humpata mtu yeyote bila kujali umri wala jinsia.

Dalili za uti
Sababu Za Kupata Ugonjwa Huu

Ugonjwa wa UTI unaweza kusababishwa na vijidudu vya namna nyingi. Bakteria aina ya Escherichia Coli kwa kiasi kikubwa ndo wanaosababisha ugonjwa huu wa UTI japo bakteria wengine wapo.


Kwa  wanawake, tatizo la fangasi katika sehemu za siri imekuwa ni tatizo kubwa sana. Uwepo wa fangasi hasa kwenye uke na maeneo jirani pia huweka mazingira ya  bakteria kuvamia maeneo hayo na kuleta maradhi ya UTI.

Kuna Lower UTI na hii ni hatua ya ugonjwa kushambulia maeneo ya kibofu cha mkojo (bladder). Katika hatua hizi, utasikia dalili kama:

– maumivu wakati wa kukojoa

. Maumivu ya sehemu za nyuma kwa wanaume

. Mkojo wenye rangi ya chai

. Maumivu wakati wa kukojoa

. Kujisikia kukojoa mara kwa mara lakini kutoa mkojo kidogo tu

. Maumivu ya kiuno kwa wanawake

. Mkojo wenye harufu kali

. Damu katika mkojo

maumivu ya tumbo chini ya kitovu na au mgongo kwa chini.

dalili za uti

Ukishazona dalili kama hizi basi ujue tayari kuna hati hati ya kuwa una ugonjwa wa uti Kitu muhimu ni kwamba usianze kutumia dawa ya aina yoyote kabla hujapimwa na daktari. Hapa ndio watu wengi huwa wanakosea na kupewa dawa ambazo huwa haziendani na hali waliyonayo. Ni vema ukapimwa kwanza ndio utapewa dawa zinazositahili.