Chanjo Kwa Watoto

Chanjo zinasaidia kumtengenezea mtoto kinga mwilini kupingana na maradhi. Chanjo hizo zinaendana na umri baada ya mtoto kuzaliwa afikishapo ️Miezi 2,️ Miezi 4,️ Miezi 6, ️Miezi 12,️ Miezi 18 . Atakapofika miaka 4-6 atachomwa tena.

️Kuna hatari kubwa mtoto alie chini ya miaka 5 ️️kukosa chanjo na wengi wao hufariki kwa haraka sababu ya kupata maradhi na miili yao haina kinga dhidi ya maradhi. Mzazi inakubidi uhakikishe mtoto amepata chanjo tangu akiwa na miezi 2 mpaka miaka 5! Ulizia vituo vya afya utapewa maelezo zaidi ni mda gani wanatoa chanjo kwa watoto.

Jamii yetu ya Tanzania inabidi tuache imani potofu juu ya kukwepa chanjo na kuhofia zinasumu,unaweka maisha ya mtoto hatarini iwapo umetokea ugonjwa wa mlipuko kupona yake ni ngumu sana ️Au akapata maradhi tu yoyote uhai wake upo mashakani.

Aina Za Chanjo

-Hepatitis B
-Robela
-Tetenus
-Surua
-Polio