Chango Kwa Watoto Wachanga (Colic)

Watoto wachanga wanasumbuliwa na chango(colic) wanapokuwa na umri wa wiki 2 baada ya kuzaliwa ndipo wanapata chango. Chango ni maamivu makali ya tumbo anayopata mtoto na kulia mara kwa mara ikiwa usiku , mchana au jioni, anaweza kulia zaidi ya msaaa 3 kwa mfululizo .

Chango inachukua mda wa miezi 3-4 ndio mtoto apone, ingawa sio watoto wote wanapata na tatizo la chango.

Sababu Za Kuleta Chango Kwa Mtoto?

 • Maziwa ya ngo’mbe yana protein nyingi , lactose inayopatikana kwenye baby formulas .(hayo yote yanaweza mletea allergy na maumivu ya tumbo
 • Mtoto atakapo nyonyeshwa sana mpaka kuvimbiwa (overfeeding) huchochea chango.
 • Hormones- zinachochea kumletea maumivu ya tumbo (mtoto akiwa na stress ya mazingira au mama anaposhindwa  kumweka position nzuri wakati wa kunyonya)
 • Gesi – Mtoto akiwa analia au kunyonya kwa haraka  anameza hewa inayokuja kuleta gesi na  kumuumiza  tumbo.
 • Kiungulia (heartburn)

Dalili Ya Chango Kwa Mtoto (colic)

Mtoto atalia sana kilio chake kitakuwa tofauti na kile cha kawaida akiwa na( njaa au usingizi au akiwa kajisaidia n.k). Analia sana akijikunja tumbo kunyoosha miguu au  vidole uso utabadili rangi na kuwa mwekundu pia anaweza kujamba mara kwa mara.

Utamsaidia Vipi Mtoto

 • Mama unatakiwa kuacha kula baadhi ya vyakula kwa kipindi hiko cha miezi 3-4 ambayo inamsumbua mtoto na chango kama (kabichi,maziwa yango’mbe au nido, cheese, kahawa, broccoli, maharage.
 • Baada ya kumnyonyesha mweke begani na mpige pige mgongoni ili abeuwe itamsaidia
 • Mama unapo nyonyesha mtoto hakikisha mtoto anaingiza mdomo kwenye chuchu yote na kufunika ule mstari mweusi bila kuacha nafasi akaingiza hewa tumboni.
 • Mfanyie massage ya tumbo – tumia mafuta ya maji weka mkononi sugua viganja vyako vikipata joto mpake tumboni kuanzia juu kuja chini litasaidia na gesi zitatoka.
 • Weka maji vuguvugu kwenye beseni na mweke mtoto akae kwa dakika 10-15.
 • Weka maji vuguvugu kwenye chupa ya plastik funika na taulo mwekee mtoto tumboni (hakikisha – maji yasiwe ya moto sana ukamuunguza.
 • Mbebe mtembee tembee au kama kunakiti chake kile cha bembea mweke abembe atanyamaza.
 • Mtoe nje apate fresh air
 • Mtoto akilia sana washa¬† au radio sometimes inamfanya anyamaze.
 • Mbadilishie maziwa ya aina nyingine kama unampa ya kopo (baby formula)
 • Usimlishe sana mpaka akavimbiwa(overfeeding)
 • Kuna dawa za colic

Tiba

Kuna dawa za  aina tofauti ila usimpe kabla ujaonana na daktari kwani mtoto ni mdogo sana huyo anahitaji uangalizi wa hali ya juu. Soma vipimo vya dawa utakavyopewa kabla ujampa mtoto.