Butterbut Squash;Lishe Ya Watoto Kuanzia Miezi 6 Na Kuendelea

Butternut squash ni jamii ya maboga ila hili linavirutubisho zaidi na ndio mana madaktari wengi wa watoto wanashauri mtoto apewe butternut squash akifika miezi sita muda sahihi wa mtoto kuanza kujifunza kula.

 

image

Umbo lake lipo kama kibuyu ,butternut ni chakula chepesi na laini kwa mtoto anaenza kufunzwa kula solid food ,lina lainisha tumbo na kumfanya mtoto kupata choo kwa urahisi kwa wale watoto wenye matatizo ya choo (constipation )linafaa zaidi.

 

 

 

Jinsi ya kupikwa

Butternut squash linanjia nyingi za kupikwa hapa nitakupa baadhi ya recipes unaweza mwandalia mtoto ,ukampumzisha kula viazi kila siku

 

  • Chemsha kwa dakika 10-15 likiiva mwaga maji weka maziwa ya baby formula (kopo) au maziwa ya mama nusu kikombe baada ya kukamua (pump) saga pamoja tayari kuliwa.

 

  • Butternut squash changanya na carroti 1 chemsha pamoja ikiiva saga na tayari kuliwa

 

  • Viazi vitamu changanya na butternut squash chemsha pamoja na kusaga

 

  • Zucchini chemsha pamoja na butternut ikiiva saga tayari kuliwa

HILI NDIO ZUCCHINI LINAUMBO LA TANGO
HILI NDIO ZUCCHINI LINAUMBO LA TANGO
  • Butternut,kiazi ulaya,karoti na njegere kidogo pika pamoja weka butter au olive oil kidogo ikiiva saga tayari kuliwa.

 

Utakapo pika chakula cha mtoto tumia butter au olive oil kwa watoto walio chini ya mwaka 1