Adhari Ya Kupasuka Chupa Ya Mama Kabla Ya Wiki 37

Chupa ya maji ya mama mjamzito – Maji yanayomzunguka mtoto kwa jina la kitaalamu yanaitwa Amniotic fluid,maji hayo yanayoshikiliwa na membrane au tissue  zinazo shikilia hayo maji kwa kipindi chote mpaka  muda utakapofika wa mama kijifungua.Hizi tissue (membrane) zinopasuka ndipo maji yanamwagika na mama anahisi kutokwa maji mengi ukeni kama mkojo.

 

 

Sababu zinazopelekea chupa ya mama kupasuka kabla ya muda wake

Chupa ya mama inaweza kupasuka kabla ya mama kupata uchungu wa kujingua .Sababu zinazopelekea

:Kama mama alishafanyiwa upasuaji kwenye njia za uzazi basi anahatari ya chupa kupasuka kabla ya muda wake.

:Infection -kama mama ana infection ya ukeni au kwenye mlango wa kizazi chupa itapasuka

:Uvutaji wa sigara

 

 

:Mama mwenye matatizo ya high blood pressure -anahatari kubwa ya kupasuka kwa chupa kabla ya muda wake vizuri kuhudhuria clinic mara kwa mara na kuchukua vipimo vya pressure.

:Mimba ya watoto mapacha – mapacha wanasababisha msukumo mkubwa kwenye membranes na chupa kupasuka kabla ya muda wake.

KAZI YA AMNIOTIC FLUID (MAJI KWENYE CHUPA YA MAMA)

 

Amniotic fluid ni muhimu sana kwa mtoto ,yanatengenezwa kwenye mwili wa mama mimba akiwa na miezi 4 .Umuhimu wa haya maji ni

:Kumpa kinga mtoto-kumwepusha na maradhi ya infection

:Kumpa joto na kulihifadhi

:Inamsaidia kwenye mmeng’enyo na upumuaji wa mtoto

 

NINI KIFANYIKE IWAPO CHUPA YA MAMA IMEPASUKA? 

Chupa ya mama mjamzito ikipasuka kabla ya wiki 37 ( premature rapture of membranes),  ni hatari inakubidi uwahi hospital upate msaada mapema sababu una hatari kubwa ya kupata infection na uhai wa mtoto unakuwa hatiani. Daktari ataangalia hali yako na kuchukua vipimo wanaweza wakakua bed rest au  wanaweza kukuanzishia uchungu ili  ujifungue kama mimba itakuwa zaidi ya wiki 34,Iwapo utaambiwa urudi nyumbani utapewa antibiotic vidonge au kuchomwa sindano ya asteroid inayomsaidia mtoto kwenye ukuaji wa mapafu

Epuka 

Pindi chupa ya maji inapopasuka mama anatakiwa kuepuka baaadhi ya vitu kama

:Kutumia vyoo vya public na iwapo utatumia kuwa makini sana ,

:Usifanye mapenzi kwa kipindi hiko mpaka utakapo jifungua ,

:Usivae tampons

.Usijiweka vidole ukeni

:Usioge kwenye tub bath au kuogelea kwani vyote hivyo vinaasilimia kubwa ya kukupa infection.

 

Amniotic fluid

Chupa ya maji ikipasuka maji yake hayana rangi wala harufu, iwapo ukaona rangi ya kijani  au brown na harufu hiyo itakuwa ni infection au mtoto kajisaidia (kunya ),rangi ikiwa nyekundu ni umebleed wahi hospital.

 

 

 

Kwa mama mjamzito aliepitisha wiki 36 chupa ikipasuka wahi hospital ataanzishiwa uchungu ajifungue  au kufanyiwa C-section kulingana na afya ya mama ilivyo kwa kipindi hiko.