Vitu Vya Kuzingatia Kabla Ujarudi Kazini Baada Ya Kujifungua

Mama anatakiwa ajipange vizuri kabla ya kurudi kazini.Huwa inakuwa ni wakati mgumu kidogo kwa mama  kurudi kazini na kuacha kichanga chake nyumbani.

 

Kawaida kuanzia week sita baada ya kujifungua ndio mda ambao huwa  unaweza kurudi kazini iwapo unahitajika kwa haraka kazini. Ila mama anahaki ya kupata miezi yake mitatu kamili ya materniy leave ikiisha ndio arudi kazini. Kuna baadhi ya wanawake wanaweza kujisikia kuwa wanahitaji kurudi kazini mapema sana baada ya kujifungua na hii inategemea na uhitaji wa kazi zilizopo na uwezo wa watu wa kumsaidia nyumbani.

Kama nyumbani una watu wa kukusaidia basi unaweza kurudi kazini mapema. Wakati unapanga likizo ya kujifungua hasa kama ni mtoto wako wa kwanza usidhanie kuwa itakua rahisi tu na unaweza kukaa nyumbani kwa mda mrefu, yaani kuna wakati utajikuta huwezi kufanya kazi  huku unamhudumia mtoto.

 

Sasa wakati unajaribu kujiuliza ni mda gani unaweza kurudi kazini baada ya kujifungua basi jiulize haya maswaali kwanza….

Unafanya kazi kwa masaa mangapi kwa siku?

Kuna umuhimu wa kuongea na boss wako juu ya masaa ya kazi. Kama unafanya kazi  masaa machache kwa week hapo itakuwa vizuri zaidi.Ukifanya kazi nusu siku  inakuwa rahisi kuwahi kurudi nyumbani na kumnyonyesha mtoto na kumhudumia .

Kama unafanya kazi  masaa 20 kwa week na ukarudi kazini kabla ya week sita basi utakua unajiletea balaa na  hatari kwenye mwili wako. Unahitaji kupumzika na kupona kwanza kabla hujarudi kazini.

 

Je una maziwa ya kutosha?

Kabla ya hujawaza kurudi kazini unatakiwa kujua kiwango cha maziwa ulichonacho,kuweza pump na kumwachia mtoto nyumbani.Kwavile mtoto bado ni mchanga yupo chini ya miezi 6 lazima apate maziwa ya mama kila siku.Unatakiwa upump maziwa kila siku kabla ujaenda kazini atakayopewa mtoto.Kumtosheleza mpaka utakapo rudi kutoka kazini.Iwapo kiwango chako cha maziwa ni kidogo unaweza kutumia mbegu za maboga kwenye vyakula unavyotumia au vinywaji ili kukuongezea uzalishaji wa maziwa.

 

Je afya ya mtoto ni salama?

Iwapo unawatu salama wa kumwangalia mtoto kwa umakini zaidi hapo unaweza mwacha mtoto nyumbani. Ila afya ya mtoto ni muhimu usikimbilie kwenda kufanya kazi wakati afya ya mtoto ipo hatari.Watoto wadogo ni rahisi sana kupoteza uhai kama mlezi hayupo makini.Na mardhi Yao ni ya gafla sana.

 

Je Kazi yako inahitaji nguvu?

Kama kazi yako huwa inahitaji nguvu au kubeba vitu vizito basi kwa kweli inabidi utulie tu mpaka week sita zipite ndio urudi kazini. Vile vile kama unatumia nguvu sana kazini, na ukirudi nyumbani unaweza kukosa nguvu hata za kumbeba mtoto anyonye na pia kabla ya week sita yaani hata mwili wenyewe unakua hauko tayari kwa aina hizo za kazi kwa hiyo unaweza kuwa unajiumiza mwenyewe.

 

Usalama wa afya yako umejifungua kwa njia gani?

Vizuri pia kuzingatia kama ulijifungua kwa operation basi unahitaji muda zaidi ili kidonda chako kipone.Nahata kama ulichomwa zile sindano za Epidural basi utajiweka hatiani na afya yako haswa upande wa mgongo. Unahitaji ujipe muda zaidi kupumzika hata week 8-12 hapo mpaka mwili utakapokuwa umekaza.

Unaweza kupata mda wa kupumzika kama ukihitaji?

Wanawake wengi huwa wanahisi wanahitaji kupumzika mida ya mchana. Kama uko nyumbani unaweza kufanya kazi zako hapo mda wowote tu unaweza kuamua mwenyewe kupumzika hata masaa kumi. Sasa huko ofisini kuna sehemu utapata angalau mda wa kupumzika na boss akakuelewa!? Kama unajua kabisa ofisini hawatakuelewa wakikuona unalala basi mama wewe tulia tu mpaka week sita ziishe na pale utakapoona mwili unaruhusu kurudi kazini, we rudi tu ukaendelee na kazi.

Chamuhimu mama  lazima kuweka  mipango yako mapema kabla ya kuamua kurudi kazini. Usipokuwa makini  unaweza kujikuta unashindwa kulea mtoto wako ipasavyo na kumyonyesha mtoto wako vile inavyostahili.

 

Please follow and like us:
error0

About afyaborakwamtoto

Hii ni Blog maalumu inayotoa elimu juu ya mambo ya uzazi na malezi bora kwa mtoto.

View all posts by afyaborakwamtoto →