Vipimo Muhimu Kwa Mama Mjamzito Kwa Kipindi Chote Cha Miezi 9

Mama mjamzito anapaswa kuwa makini sana kwa kipindi chote cha miezi 9 . Kuhakikisha ana hudhuria klinik(prenatal care) bila kukosa  ili kufatilia ukuaji wa mtoto ,iwapo mama mjamzito amepata tatizo ni rahisi kusaidiwa mapema na kuokoa uhai wake na wa mtoto .

 

 

image

Mama huchukuliwa vipimo vya mimba kwa wakati tofauti kuna baadhi hujirudia hupimwa mara kwa mara kuna vile ambavyo hupimwa miezi mitatu ya  mwanzo wa mimba(first trimester) kuna vya miezi ya 3 ya katikati (second trimester) na vya miezi mitatu ya mwisho(third trimester).Sababu mtoto hukuwa kila siku na kufanya mabadiliko makubwa ni muhimu kufatilia kwa makini kwa kila kipimo.

 

Vifuatavyo ni vipimo muhimu kwa mama mjazmito kwa kipindi chote cha miezi tisa ya mimba yake.

  • Kiwango cha damu

  •  Kupimwa kiwango  cha damu mara kwa mara ni muhimu, kipindi cha ujauzito wa mama wengi wanapata tatizo la upungufu wa damu(Anemia in pregnancy) ,damu ikipungua mwilini mama anakuwa na hatari kubwa ya kifo au kuzaa mtoto kabla ya mda wake.

    anapopungukiwa na damu anahitaji kutumia dawa na kula matunda au  vyakula vya kuongeza damu mwilini kama(beetroot,nyanya,parachichi,kiwi,nanasi,limaochungwa,boga,viazi vitamu,matembele,spinach maharagwe,samaki ,nyama,njegere na dagaa)n.k

 

image

STds/HIV
Magonjwa ya zinaa na upungufu wa kinga mwilini(ukimwi) huathiri ukuaji sahihi wa mimba. Magonjwa haya ni kama syphilis, gonorrhea, herpes, chlamydia and hepatitis B na C na upungufu wa kinga mwilini (ukimwi).
Kugundulika kwa magonjwa ya zinaaa mapema kwa mama mjamzito ni muhimu kwani maradhi haya huleta adhari kwa mtoto tumboni na wakati wa kuzaliwa. Hivyo mama awazeka kupewa matibabu haraka na kuzui maambukizi kwa mtoto.Dalili za magonjwa ya zinaa anapojisikia anamabadiliko ya mwili kama (kutokwa maji maji yenye harufu kali,kupata maumivu wakati wa haja ndogo)na maumivu ya tumbo chini ya kitovu ),anapata vipele,kupungua uzito,kukosa hamu ya kula,homa za mara kwa mara,kikohozi kisichoisha wahi hospital haraka . Maradhi kama syphils na ukimwi huweza athiri mtoto akiwa tumboni ni vizuri mama kupewa kinga ili mtoto asipate mashambulizi.

image

Magonjwa kama chlamydia, gonorrhea, hepatitis B na genital herpes huweza mpata mtoto wakati anasogea katika shingo ya uzazi ili aweze toka nje.(wakati wa kuzaliwa).
Magonjwa ya zinaa husababishia mtoto upofu,uziwi, azaliwe kabla ya wakati, uzito mdogo,na kusababishia kifo kwa mtoto.

Kipimo cha mkojo
Huonyesha hali ya afya ya mama mjamzito  katika maswala ya maambukizi ya bacteria, UTI na matatizo katika figo za mama.Hivyo ni muhimu kwa mama mjamzito kupimwa mkojo kwa wakati wote wa mimba.

uwepo wa kiwango kikubwa cha sukari katika mkojo wa mama hutokana na hormone kuzuia insulin kutoa sukari katika damu. Mara nyingi hii hutokea katikati ya kipindi cha pili cha mimba,hali hii huweza kutibiwa kwa mama kupewa lishe maalumu kwa kipindi chote cha mimba mbaka pale tatizo litakapo isha.

 

Kupima pressure
upimwaji wa presha wakati wa mimba ni muhimu sana ukizingatia matatizo ya pressure huja na mambo mengine mbalimbali. pressure hupelekea kifafa cha mimba  na kifafa cha mimba hupelekea athari kama kifo kwa mama na mtoto

kifafa cha mimba hupimwa kwa kuangalia katika damu na uwepo wa protein katika mkojo. ivyo ni muhimu mama mjamzito kukumbushia kipimo hiki kila ahudhuriapo klinik.

 

Ultra sound
kipimo hiki hufanyika kila tremester ya mimba na ni muhimu kufanyika kwani

  • ukuaji wa mimba,

  • husaidia kujua kama kuna tatizo lolote lile la ukuaji katika mimba.

  • husaidia kujua umri wa mimba na jinsi ya mtoto

  • Kuskiliza mapigo ya moyo ya mtoto

 

image

 

 

Upimwaji wa malaria
malaria ni hatari kusababisha kifo,kuharibu mimba(miscarriage) vizuri kupima na kutumia kinga kama net pindi alalapo.

Please follow and like us:
error0

About afyaborakwamtoto

Hii ni Blog maalumu inayotoa elimu juu ya mambo ya uzazi na malezi bora kwa mtoto.

View all posts by afyaborakwamtoto →