Utando Kwenye Kichwa Cha Mtoto (Cradle Cap)

Utando kwenye kichwa cha mtoto mchanga ,wengi mnalijua hili sio geni kwa watoto wachanga kupata layer flani ivi kavu sana yenye kuipa rangi nyeupe au njano.Ni kawaida  kwa watoto wachanga japo inaweza mfanya akajikuna sana nakumfanya kuwa discomfort.

image

 

Madaktari wengi wa watoto wanasema hakuna kitu cha moja kwa moja kinacho sababisha mtoto kupata hiyo hali (cradle cap ) kiitalamu wanaita infantile sebborheic dermatisis ,madaktari wengine wanaona ni mabadiliko ya hormones anayopata mtoto kutoka kwa mama yake huchangia .

image

Utando huu huwa unajitokeza maeneo mengineo ya mwilini pia kama masikioni,juu ya nyusi (eye brows) na makwapani,hii hali inawashika watoto kwa kipindi tofauti wengine kwa muda mfupi tu wengine kwa miezi 6-12 inategemea na ngozi ya mtoto.

 

 

Tiba

 

Tiba yake ni asilia tu utakayo ifanyia nyumbani kutumia vitu asilia kama

  • Mafuta ya nazi -tumia maji vugu vugu unapomwogesha kichwani tumia sabuni au mild shampoo mwekee kichwani sugua kwa mkono wako,mswaki laini au  brush  taratibu then mwagie maji ,mkaushe na kumpaka mafuta ya nazi yawe ya kutosha tumia kitana chake kisicho na makali mchane taratibu utaona ukoko unatoka taratibu fanya hivyo mara 1-2 kwa siku kila akioga.

image

 

 

 

  • Olive oil -nayo ni asilia na mazuri kwa watoto unaweza tumia baada ya kuoga au hata bila kuoga chukua kitaulo lowanisha maji pitisha kichwani kwake then mpake olive oil  baada ya dakika 10-15  mchane utaona inatoka.

image

  • Tea tree oil ,baby johnson na almond oil nayo unaweza kutumia .

  • Mafuta ya mgando au baby Johnson nayo yanafaa.

Please follow and like us:
error0

About afyaborakwamtoto

Hii ni Blog maalumu inayotoa elimu juu ya mambo ya uzazi na malezi bora kwa mtoto.

View all posts by afyaborakwamtoto →