Upungufu Wa Damu Kwa Mama Mjamzito,Dalili Na Matibabu

Hili ni  ️tatizo la kawaida kwa wamama wajawazito kupungukiwa damu mwilini kipindi cha ujauzito !hii inatokana na mwili kuhitaji damu nyingi kwa ajili ya ukuaji  wa  ️mtoto,tatizo hujitokeza  kipindi cha miezi mitatu ya mwisho (third trimester).

 

image

 

upungufu wa damu kwa mama ️ mjamzito upo wa aina 3 tofauti

 • Iron -deficiency anemia-ni upungufu wa madini ya chuma- ambao una sababisha kuzalisha kiwango kidogo sana cha damu.

 

 •  Folate -deficiency anemia. Mama anakuwa na upungufu wa damu unaotokana na kukosa folic acid mwilini ambayo inasaidia Kwenye utengenezaji mpya wa cells na uzalishwaji wa red blood cells ,mama aliekosa folic acid anaweza kuzaa mtoto mwenye mapufungu kama kuzaliwa mgongo wazi au kichwa kikubwa hivyo mama anatakiwa kumeza vidonge vya folic acid kipindi cha  miezi 3 ya mwanzo mwamimba.

 

 • VitaminsB12 deficiency anemia- mama anakuwa na ukosefu wa vitamini b12 inayohitajika kwenye uzalishaji wa chembe hai nyekundu(red blood cell) .Mlo wa mama unapokuwa sio kamilifu unaweka hitilafu ya kuzalishwa kwa chembe nyekundu na kuadhiri uzalishwaji wa damu ,mama anatakiwa kula nyama,kuku,maziwa na mayai ili kusaidia kuzalishwa kwa damu mwilini.

 • image

 

 • Dalili kwa upungufu wa damu mwilini

 • Kusikia kizungu zungu

 • Kukosa nguvu

 • Kubadilika rangi ya mwili kuwa mweupe kuliko kawaida , utaona viganjani,kwenye kucha ,macho na ulimi

 • Kukosa umakini wa kuona vizuri

 • Mapigo ya moyo Kwenda mbio

 • kushindwa kupumua vizuri

 • Kuvimba miguu

 

 

Adhari za upungufu wa damu kwa mama mjamzito

mama mjamzito anakuwa na hatari kubwa ya kupoteza uhai wake pindi ajifunguapo,sababu zoezi zima la kujifungu linahitaji damu ya kutosha ,akipoteza damu nyingi ni hatari kwake kuishiwa damu mwilini. Upungufu wa damu kwa mama humwadhiri mtoto tumboni na

 • Kuzaliwa mwenye afya dhoofu alie na uzito mdogo.

 • Mtoto kuzaliwa kabla ya mda Wake(njiti)

 • Mtoto kuwa na upungufu wa damu

 • Mtoto kuzaliwa kiwa amechoka (fetal distress)

 • Mtoto ukuaji Wake unadumaa ,stage za ukuaji unakuwa mbaya na kuadhiri maendeleo duni ya kiakili.

 

 

Wamama wenye hatari ya kupata tatizo la upungufu wa damu (anemia)

 • Wenye kushika mimba zaidi ya mtoto mmoja (mapacha)

 • Mimba za utotoni

 • Wenye matatizo ya upungufu wa damu kabla ya kushika mimba

 • Kushika mimba kwa haraka baada ya kujifungua mtoto mwingine

 • Wanao kula lishe isijitosheleza kwenye madini ya chuma

 

Tiba

Upungufu wa damu unaweza tibika kwa haraka na kuokoa maisha ya mama na mtoto ,kinachotakiwa mama anahitaji kupima kiasi cha damu kila ahudhuriapo klinik.Na anaweza kuongeza damu kwa kutumia vidonge vya madini ya chuma kwa miligram 2-4.8 kwa siku.

 • Kutumia vidonge (supplements) za folic acid zinasaidia kuongeza kiasi cha damu kwa haraka

 • Tumia matunda ya beetroot unaweza yachemsha ukatengeneza juice , unanweza ukasaga ukanywa au ukapikia kwenye chakula zinapatikana masoko ya kisutu aua kariakoo sokoni kwa bei kati ya 3000-5000 Tshs hapo.

 

image
matunda ya beetroot
 • Kula matunda kwa wingi, tafuna au kunywa juice ya nyanya

 • Tumia juice ya rosella glasi 2-3 kwa siku

 • Kula mboga za majani spinach,mchicha,brocoli au matembele kwa wingi

 • Kula dagaa au kunywa supu ya maharagwe kwa wingi

 • Kula nyama,kuku na samaki

 • kunywa maziwa ,cheese na kula mayai

 

 

Ushauri toka kwa afyabora kwa mtoto.

Zingatia kupima kiasi cha damu mara kwa mara uendapo klinik, ni hatari kupungukiwa na damu hata kama ni kiasi kidogo kipindi chote cha ujauzito.

 

Please follow and like us:
error0

About afyaborakwamtoto

Hii ni Blog maalumu inayotoa elimu juu ya mambo ya uzazi na malezi bora kwa mtoto.

View all posts by afyaborakwamtoto →