Umuhimu Wa Kubeuwa Kwa Mtoto Mchanga Baada Ya Kunyonya

Watoto  wachanga wanaonyonya maziwa ya mama wengi  hawapati tatizo la gesi kwa wingi kama watoto wanaokunywa maziwa ya kopo (baby formula) ,sababu mtoto anaponyoya kwa chupa anaingiza hewa tumboni kwa wingi na inakuja kumuumiza tumbo. Ila mtoto anaenyonya ziwa la mama ni kiasi kidogo cha hewa kinachoingia tumboni.

Watoto wanatakiwa wasaidiwe kubeuwa baada ya kunyonyeshwa.  Inamsaidia

:Kutoa gesi baada ya kunyonya

:Kumwepusha na maumivu ya tumbo

:Kumwepusha kucheuwa na macheuwo kupitia puani

 

Mtoto anapomaliza kunyonyeshwa mweke begani ,mpige pige mgongoni taratibu kwa dakika chache mpaka umsikie amebeuwa(kutoa gesi). Epuka kumlaza kabla haja beuwa – kucheuwa baada ya kumnyonyesha sababu akicheuwa yatapitia puani na kumfanya ashindwe kupumua na kupata maumivu makali.

 

Nimuhimu umbebe kwa dakika 10-20 ndio umlaze.

Please follow and like us:
error0

About afyaborakwamtoto

Hii ni Blog maalumu inayotoa elimu juu ya mambo ya uzazi na malezi bora kwa mtoto.

View all posts by afyaborakwamtoto →