Umri Wa Kumpeleka Mtoto Day Care

So umeshajifungua mtoto na unafurahia  tayari ameshaanza kutembea na hata kukimbia, ila sasa swali linakuja je  ni umri gani  wa kumpeleka mtoto day care. Katika hali ya kawaida unaweza kuwana mtoto na bado ukawa unafanya kazi na ukajikuta unatakiwa kupata usaidizi kidogo kuhusu mtoto. Sasa ukiangalia hauna mfanya kazi wala ndugu wa kusaidia na kwa hali inavyoendelea unaona ni bora tu ukampeleka mtoto wako day care centres. Ila sasa kwanza kabisa  ni umri gani mtoto anatakiwa kupelekwa day care.

Umri wa kumpeleka mtoto day care centre unatakiwa   angalau akishafikisha umri wa mwaka mmoja au mmoja na nusu. Yaani huo umri ndio unamkua ni mzuri zaidi kuliko akiwa chini ya mwaka mmoja. Mtoto akishafikisha mwaka mmoja huwa anakua tayari na ule uelewa wa rugha na mambo mengine yanayomzunguka, na kitu ambacho kinafanya huu umri kuwa ni mzuri ni kwasababu mtoto anakua tayari ameshaanza kutengeneza mahusiano mazuri kati yake na mama yeke na wazazi na hata ndugu wanaomzunguka tayari anakua na ule uzoefu wa kukutana na watu tofauti tofauti kwa hiyo unapo mpeleka mtoto mwenye umri wa kuanzia mwaka mmoja na nusu basi hapo unakua ni umri sahihi kwa yeye kukutana na watu wengine.

Mtoto akishafikisha mwaka mmoja tayari anakua ameshapitia ile misuko suko ya kutengana na wazazi wake hatua ambayo huwa inaanza akishafikisha umri wa miezi tisa kwa hiyo ukimpeleka day care hatokua na tatizo la kutengana na wazazi wake.

Kwa watoto ambao ni chini ya mwaka mmoja uwezo wa kuwapeleka unao kwa sababu ni wewe tu kama mzazi kuamua kumpeleka ila kipindi hiko mtoto huwa anahitaji uangalizi wa karibu sana kila mara na mara nyingien bada wanatatizo la kutengana na mama yake kwa hiyo yaani inaweza kuwa ni tatizo kwa hao watu utakaowapelekea.

Umri Gani Mzuri Kumpeleka Mtoto Day Care

Tips za Kuchagua Day Care Nzuri

Kuna mambo mawili muhi ya kwanza ya kuangalia  kituo cha kumpeleka mtoto wako:

Usalama Kwanza

Hii ni hatua ya kwanza ya kuangalia kama mahali ambapo wanatakua wanashinda kuna usalama wa kutosha. Maana kama day care haina usalama wa kutosha unaweza kwenda siku mmoja unakuta mtoto wako hayupo na watu wengine wanachukua watoto wao, kwa hiyo kuna hati hati ya watoto kupotea.

Usafi

Usafi ni jambo linguine ambalo utakiwa kulichunguza sehemu ambayo unataka kumpeleka mtoto wako. Watoto wengi wakishaenda day care centres ndio hapo wanachangamana na watoto wengine sasa hii kwa namna nyingine ndio nyingine ya mtoto  kupata magonjwa mbalimbali kwa hiyo kama kituo hakina njia nzuri za usafi basi watoto hapo watakua na balaa. Hii ni pamoja na kujua ni chakula gani wanapatiwa hapo kituoni na kma mtoto wako ana alegi ya vyakula faln huo ndio mda wa kuwaeleza kabisa mapema.

Baada ya hivyo vitu sasa ndio unaweza kuangali sasa ni mambo gani wanafundisha watoto wanapkua hapo, ni vitu ambavyo watoto watakua wanafanya kwa mda wote wa siku nzima, yaani ratiba kamili ya siku inabidi uwe unaifahamu  vizuri ili uwe unaelewa kabisa mwanao kwa asa anafanya nini sio unamuweka mtot kwenye kituo na wala hata hujui ratiba nzima ya siku ikoje.

Please follow and like us:
error0

About afyaborakwamtoto

Hii ni Blog maalumu inayotoa elimu juu ya mambo ya uzazi na malezi bora kwa mtoto.

View all posts by afyaborakwamtoto →