Uji wa watoto Kuwanzia Miezi Sita

Uji ni lishe nzuri kwa watoto waliofikisha miezi sita na kuendelea! Mzazi unatakiwa umpikie uji wa aina tofauti ili asikinai mapema,sababu utakapo mpa uji wa aina moja lazima atauchoka na kuukataa!

  • Unaweza tumia nafaka tofauti kutengeneza uji ,Taasisi ya afya na lishe wanashauri   mtoto alie chini ya miaka 5 hawezi tengenezewa nafaka nyingi kwa pamoja ,nafaka zisizidi  mbili mfano mahindi na mchele au ukamsagia mahindi peke ikawa moja.

 

image
Mahitaji
image
Tayari kubandika

 

UJI WA MCHELE.

  • tuone jinsi ya kuandaa uji wa mchele

??MUDA 30dk

Mahitaji

  • Mchele robo kikombe

  • Apple 1

  • Ndizi mbivu 1 (iliyoiva tayari kuliwa)

  • Siagi/butter kijiko 1 cha chai

  • Nutmeg (Kungumanga) robo kijiko -inamsaidia mtoto Kwenye ukuaji wa ubongo.

  • Maziwa kikombe 1

Jinsi ya kupika.

Pembua na kusafisha mchele kwa Maji safi ,weka kwenye sufuria na katia vipande vidogo vidogo vya apple hakikisha umelimenya kabla ujaweka.

Ongezea ️Maji kikombe 1 funika weka na nutmeg ,bandika jikoni moto usiwe mkali baada ya dakika 25 epuwa kikiwa kimeiva.

Wacha kipoe ,weka Kwenye blenda ,ongezea ndizi mbivu 1 na maziwa pamoja na siagi saga kwa pamoja .Usitumie sukari ndizi ndio unaitumia kama sukari.

Kitakuwa tayari kuliwa baada ya kupoa.

 

 

OBS:Kungumanga inafaida nyingi mwilini ,wengi wanatumia Kwenye vyakula vyenye sukari,ila usimwekee nyingi kipimo ni robo kijiko kwa mtoto ukimpa nyingi itamfanya alale sana.

Please follow and like us:
error0

About afyaborakwamtoto

Hii ni Blog maalumu inayotoa elimu juu ya mambo ya uzazi na malezi bora kwa mtoto.

View all posts by afyaborakwamtoto →