Tips Zitakazokusaidia kama Mtoto Akilia Baba Anapomgusa.

Mtoto Akilia Baba Anapomgusa

Tuseme ukweli hii hali ya mtoto akilia baba anapomgusa huwa inaleta utata hasa pale mwanzoni.  Mtoto akizaliwa huwa anatumia mda mwingi sana na mama yake. Hii huwa ni kawaida kwa sababu ndio inavyotakiwa yaani ni kawaida hivyo kuwa anatakiwa kuwa na mama karibu ili amuhudumie. Ila sasa inakuaje kama mama ana kazi na hana mtu wa kumsadia? Unawaza na kusema baba anaweza kusaidia kuwa nae. Tatizo ni kwamba Baba akimbeba tuuu, mtoto anatoa kilio cha hatari hapo  Analia mpaka mishipa inatoka ila mama akimchkua tu anakaa kimya. Sasa tunafanyaje ili huyu mtoto amzoe baba yake endelea kusoma nimekuwekea nji ambazo unaweza kuanza kuzitumia ili mtoto amzoee baba yake.

Sasa chini ni baadhi ya tips  zitakazokusaidia kama mtoto akilia baba anapomgusa

Baba Acheze Nae

Kwa mwanzo mwanzo baba awe anajaribu kucheza nae amuangalie machoni au kumshika shika wakati amebebwa na mama yake. Ukifanya hivi mtoto wako atapata confidence akiwa karibu yake. Baba sometimes anaweza kuwa anaogopesha kwa watoto na sauti yake ile ilivyokubwa  na harufu yake ni tofauti na ya mama aliyoizoea kwa hiyo anaona kabisa huyu ni mtu tofauti kabisa, na wakati mwingine unakuta baba anambeba mtoto usiku wakati amerudi kazni mtoto nay yeye kachoka kwa hiyo akibebwa na baba ambaye bado hajamzoea basi kilio chake hapoo!!

Mlale Wote

Kama usiku huwa mnalala wote basi mtoto muweke katikati yenu hii inamfanya azoee kuwa karibu na baba.

Muache Na Baba Yake.

Umeshawahi kumuacha mtoto wako na baba yake. Hii ndio njia nzuri sana ya kutengeneza mahusiano mazuri na baba na mtoto. Hii inaweza isifanye kazi mwanzoni kwa hiyo jaribu kuangalia ikifikia hatua ambayo baba akigusa halii au akimbeba basi jaribu sasa kumuacha nae kama nusu saa au saa moja af tuone kama ukirudi utakuta kilio cha hatari au utakuta kumetulia kama ulivyopaacha!

Mtoto Akilia Baba Anapomgusa

Surprise

Njia nyingine ni kumpa mtoto surprise na hii iko hivi mtoto akiwa amelala usingizi muache af mwambie baba akae karibu ili mtoto akiamka tu akutane na baba yake we usiende kwanza af usikilizie hali inaendaje kwa mwanzoni unaweza kulia ila kama mkirudia mara mbili mara tatu mtoto  atamzoea na kuona kumbe na yeye mtu mzuri kwake.

Kama ukiendelea kuwaacha waendelee kuwa pamoja iwe pamoja wewe ukiwepo au wakiwa peke yao tu bila wewe kuwepo nina uhakika mtoto atamzoea baba yake na hakutakuwa na tatizo lolote

Please follow and like us:
error0

About afyaborakwamtoto

Hii ni Blog maalumu inayotoa elimu juu ya mambo ya uzazi na malezi bora kwa mtoto.

View all posts by afyaborakwamtoto →