Tabia Ambazo Unatakiwa Kuziacha Ukiwa na Mtoto

Watoto huwa wanajifunza mambo mengi kuhusu miili yao, uwezo wao na mambo kibao kutokana na mambo unayoyafanya na kuyasema wewe  kama mama yake au baba yake.  Jinsi ya kuwafundisha watoto tabia nzuri sio kuwapa zawadi na kuwapiga wakikosea, ni kwa kuwaonyesha kwa vitendo na kuwa positive kwa kila jambo na kila tabia mpya wanayoionyesha.

Kama ukionyesha mfano mzuri kwa watoto utawaonyesha kwa njia ya uhalisia na wanaelewa zaidi na hii itawasaidia kufanya maamuzi mazuri maishani.

 

Kujilaumu mwenyewe

Tabia ya kujilaumu kila mara mbele ya watoto na kuwaonyesha madhaifu yako hiyo inaweza kupelekea watoto nao wasiweze kujiamini na kukuamini pale ambapo utawaagiza kitu. Ongelea mambo mazuri ya kwako na kama unaongea kitu ambacho kinaonyesha udhaifu wako basi ni vema kuongea nao kwa heshima taratibu, ila ukiongea ongea tuu hapo sebuleni na wenyewe wapo basi wataokota maneno ambayo baadae wakiyatumia inakua balaa mbele ya familia.

 

Kuchat, kupiga simu  kila mara

Sidhani kama mtoto wako atakuelewa kama ukimwambia aache kuchart wakati wa kula wakati wewe una simu yako mezani, na watoto wa siku hizi walivyo mh! Mungu atusaidie tu maana wakiona unafanya kitu tu, lazima wafanye. Kitu unachokifanya kinatuma message  kubwa sana kuliko kitu unachosema. Weka sheria za nyumbani na kila mtu ndani azifate. Inabidi mkiwa ndani ya nyumba mda wa familia lazima muwe na mda kidogo wa kifamilia sio kila mara kila mtu yupo na simu au computer.

 Kunywa Bia ili kupunguza Stress.

Kama unarudi nyumbani na siku ilikua sio nzuri na ukasema ehm “ngoja ninjwe mbili tatu kwanza”  ili uwe vizuri kidogo basi hiyo tabia unawaonyesha watoto kuwa bia ni njia ya kupunguza stress na kupumzika. Vile vile hata ukitumia sana kahawa au soda au energy drinks, hii watoto wajifunza kuwa akiwa hayuko sawa atakua anafanya hivyo hivyo.

Badala yake jaribu kutafuta njia nyingine nzuri za kupunguza stress, kama ndio kuchukua hizo mbili, tatu bia basi nenda kimya kimya sio lazima kusema mbele ya watoto.

Kufanya Kila Kitu ni Mashindano

Yaani usifanye kila kitu ni mashindano. Hii huwa inatokea sana kama mtoto asipofanya vizuri kwenye masomo au kwenye michezo, huwa tunapenda kuwalinganisha na watoto wengine. Mfano “Utasema mbona John kafaulu kuliko wewe” Sometimes kusema hivyo  inaweza kumfanya ajifunze, ila kama ukendelea kutumia hiyo njia kila mara na kufananisha na watoto wengina inaweza kumshusha nguvu.

Njia nzuri ni kumsifia kwanza kwa kile alichojaribu kufanya na jaribu kumuelekeza taratibu jinsi ya kujiendeleza na hata umuulize ni wapi anakwama ili akuambie wewe mwenyewe.

Kila Mara Mnabishana

Kama wewe na mwenzi wako mnabishana kila mara, watoto wenu wanajifunza kuwa kumbe wanaruhusiwa kubishana na wao. So kesho na wewe ukikuta wanabishana au wanapigana basi ujue kuwa hawajajifunza mbali ni humo humo ndani kwenu.

 

 

Stress mara nyingi husababisha au kama kuna sababu zingine mbishane, hii mnatakiwa mbishane  chumbani na wasiwasikie au mkabishanie mbali na nyumbani. Mtoke kabisa vizuri ndani muende mbali mkabishane vizuri huko illi mkirudi ndani watoto wasijue kama kuna ugonvi unaendelea ndani ya nyumba.

 

Kuongea Umbea.

Hapa sasa jamani ndio watoto huwa wanajifunza maneno ambayo hata hayaendani na umri wao. Swala la kuongelea mambo ya watu wengine jinsi wanavyoonekana, walivyovaa au wanafanya mambo gani mbele ya watoto hiyo ni njia nzuri kabisa ya kufundisha mtoto tabia za umbea na kufatilia mambo ya watu.

Kama upo na shoga yako na mnataka kuongea umbea jamani hakikisha hao watoto hawapo karibu, ila kama wapo karibu mwenzangu watajifunza mambo mengi kuliko, tena akienda kwa jirani kucheza na akakuta na huko wanapiga umbea ndio kabisa atakaa kusikiliza maana alikuona wewe mama unapiga umbea nyumbani kwa hiyo hatoona kama hiyo ni tabia mbaya.

Kukasirika mbele ya watoto

Kama umejikuta umekasirika mbele ya watoto, wala usijifiche na kutegemea kuwa hajakuona kama umeshavurugwa, we waambie tu tayari kuna mtu kakuchanganya tayari na hauko sawa. Tena kama unaweza wee waambie kisa kilichotokea kama ni sawa kuwaambia na uwaulize jinsi ya kutatua tatizo

Please follow and like us:
error0

About afyaborakwamtoto

Hii ni Blog maalumu inayotoa elimu juu ya mambo ya uzazi na malezi bora kwa mtoto.

View all posts by afyaborakwamtoto →