Smoothie Ya Ndizi Na Maziwa Kwa Afya Bora Ya Mtoto

Smoothie ya ndizi na maziwa inavirubisho vingi vizuri mwilini kama protein,fiber,vitamini,madini ya chuma,nk. Huongeza uzito , inakupa nguvu na kulainisha Ngozi ya mwili,kujenga mifupa iwe imara na faida nyinginezo nyingi.

image
MCHANGANYIKO WA NDIZI MBIVU NA MAZIWA

 

 

MAHITAJI

  • ndizi mbivu 2

  • Maziwa glas 1

  • Test ya vanilla au asali ukipenda!

 

Jinsi ya kuandaa

Menya ndizI mbivu,weka kwenye blenda, ongezea glasi moja ya maziwa na robo kijiko cha chai cha vanila utasaga pamoja ukipenda ,unaweza sagia na vipande vya barafu kwa matumizi ya mtu mzima! Tayari kutumika!

 

 

Watoto chini ya miezi 12

Mama utumie maziwa ya kopo au yakwako baada ya kukamua ili ukisaga utumie,maziwa ya ng’ombe madaktari  hawashuri kupewa mtoto chini ya mwaka mmoja wanauwezo mkubwa wa kumdhuru kutokana na protein nyingi ilipo ndani.

 

 

Please follow and like us:
error0

About afyaborakwamtoto

Hii ni Blog maalumu inayotoa elimu juu ya mambo ya uzazi na malezi bora kwa mtoto.

View all posts by afyaborakwamtoto →