Sababu Zinazo Pelekea Mimba Kuharibika(Miscarriage)

Miscarriage ni hali ya mama kupoteza ujauzito wake (kutoka) kabla ya wiki 20 kitaalamu wanaita spontaneous abortion,katika wanawake 10 wajawazito 1-2 kati yao wanaweza kupoteza ujauzito wao hiyo ni tafiti nyingi zinavyoonyesha.

image

Wajawazito wengi mimba zao huaribika kipindi cha miezi 3 ya mwanzo (first trimester).Mwanamke anaposhika mimba maratarajio ya safari yake yote  miezi 9 itakwenda salama na kufanikiwa kushika mtoto wake mikononi mwake,ila inakuja kugeuka kutokana na sababu tofauti tofauti  zinazopelekea kuharibu mimba hiyo na kukatisha ndoto zake ni maumivu makali wanayapa moyo.

 

 

Sababu zinazopelekea kuharibika kwa mimba

 

Mama anapopata miscarriage atajiuliza mimba yangu kwanini imetoka tatizo ni nini? Inakuwa ngumu daktari kujua kwa haraka nini imepelekea na ndio mama kuna wadada wengi huwa wananiandika kila wapatapo mimba zinaharibika, sasa wacha tuone vyanzo vinevyo vinavyo sababisha miscarriage  huenda utapata ufumbuzi na muda ukifika wa kushika mimba tena utajua wapi ulikuwa unakosea na utajisahihi ,sababu ni hizi

 

 • Fetus / embroy anakuwa hana mfumo mzuri wa ukuaji chromoses inakuwa haipo kwenye hali ya kawaida ni abdnomal hapo inaadhiri mfumo mzima wa mimba na kupelekea kuharibika.

 • Magonjwa sugu-mama anapokuwa na magonjwa sugu kama kisukari ,moyo au rheumatoid

 • Infection-U.T.I,magonjwa ya zinaa kama kaswende n.k epuka magongwa ya infections.

 • Mapungufu kwenye uterus-uterus ya mama inapokuwa na matatizo kama uvimbe (fibroid),makovu au vidonda,

 • Hormonal imbalance-homoni za mama zinapokuwa hazipo kwenye uwiano( balance) kunasababisha kuharibika kwa mimba

 

image

 • Uzito mkubwa (unene) / uzito mdogo unachangia mimba kuharibika na unaweza mfanya mama akapoteza maisha yake pia

 • Miscarriage zaidi ya mara 2-Mama aliepata miscarriage zaidi ya mara 2 anauwezo mkubwa wa kuharibika kwa mimba yake  kila ashikapo

 • Kutoa mimba-mwanamke anapotoa mimba mara kwa mara kizazi chake kinakuja shindwa kuhimili kubeba ile mimba kwa miezi 9,na kumfanya kila ashikapo ikifika miezi flani inatoka tu yenyewe sehemu za uzazi zinakuwa zimeshalegea

 • Matumizi ya Pombe,Sigara,Bangi,Madawa ya kulevya vyote vinaleta miscarriage.

image

 • Ajali-mama kama amepata ajali akagonga maeneo ya tumbo au kupata mshtuko mkubwa basi ni rahisi mimba kuharibika

 • Caffein -mama anapotumia kahawa  kwa wingi, soda au cocacola anaharatarisha kuharibu mimba

 • Msongo( stress)

 • Mimba za utoto au uzeeni-binti anaposhika mimba akiwa mdogo chini ya miaka 18 inahatari ya kuharimika sababu vizazi vyake havipo tayari kumudu kubeba mimba kwa miezi 9,ni sawa na mwanamke mwenye miaka 40 anahatari ya miscarriage sababu vizazi vyake havina nguvu tena za kumudu mimba kwa kipindi cha miezi 9.

 

 

 

 

Dalili ya mimba kuharibika

 

 • Kutokwa damu kwa wingi kama mabonge

 • Kusikia maumivu makali chini ya kitovu

 

image

Mama mjamzito anaweza kuona dalili ya kutokwa damu  akawahi hospital kuna vipimo  utafanyiwa cha pelvic , ultrasound n.k kuhakiki kweli mimba imetoka yote? kuwezekano wakukutwa  mimba haijaharibika vibaya , kuna aina tofauti za miscarriage nyingine haziwezi saidiwa zinatoka moja kwa moja na nyingine zinaweza okolewa  na mimba ikabaki hai kuendelea kukua mpaka miezi 9 ,cha muhimu ukiona hizo dalili awahi kituo cha afya.

 

Ushauri

 

Wadada wanatoa mimba kwa kujali ujana ila muda unapofika  wa kutaka mtoto wanakuwa hawana tena uwezo wa kushika mimba inauma sana na inasikitisha, sababu wengi wao wanatolewa mimba vibaya wanaachwa na uchafu mwisho wasiku wanapata infections zinawatafuna bila wao kujua na kuadhiri mfumo mzima wa uzazi ,hii ni hatari sana kutoa mimba ni kosa la jinai ila jua iwapo umetoa  au imeharibika (miscarriage) mimba unatakiwa kutumia

 • Antibiotic ili kuzuia infections na kukausha kidonda,

 • Epuka kufanya mapenzi mpaka baada ya wiki 5-6 kidonda kikiwa kimepona kabsa,

 • Epuka kutumia sabuni za harufu,

 • Usijiweke vidole  ukeni  wakati wa kuoga wala usitumie zile pad za tampons (KIDOLE).

 

 

2. Kwa mama anaepata miscarriage zaidi ya mara 2 jaribu kwenda kwa madaktari wazuri wa wanawake wakufanyie vipomo kujua tatizo nini,kipimo cha hormonal imbalance

 

Please follow and like us:
error0

About afyaborakwamtoto

Hii ni Blog maalumu inayotoa elimu juu ya mambo ya uzazi na malezi bora kwa mtoto.

View all posts by afyaborakwamtoto →