Sababu Zinazo Mfanya Mtoto Akatae Kunyonya

 • Maziwa ya mama ni muhimu sana kwa mtoto ,yanampa lishe na afya nzuri .Maziwa ya mama  yana virutubisho,calories na vimiminika vya kutosha.

image

 

 • FAIDA YA MAZIWA YA MAMA.

 • Mwongezea uzito kwa haraka.

 • Yana mwepusha na maradhi mengi cancer,mzingo (allergy)

 • Anaepuka kupata infection ya masikio

 • Pumu

 • Inampa kinga ya kumwepusha kuhara mara kwa mara

 

       FAIDA YA MAMA KUNYONYESHA

 • Ni rahisi yanapatikana mda wowote sio gharama.

 • Mama anaponyenyesha anapùnguza hatari ya kupata cancer.

 • Inamsaidia kuchelewesha kuona hedhi ya mama na kumfanya kutunzwa kwa madini ya chuma mwilini.

 • Itakusaidia kuimarisha mifupa ukija kuzeeka .

 

    SABABU ZINAZOMFANYA MTOTO ASHINDWE KUNYONYA

 • Anamaumivu mdomoni (vidonda)mchunguze

 • Infections ya sikio(anapata maumivu makali anashindwa kuvuta maziwa)

 • Mama unatumia mafuta au perfume yenye harufu kali.

 • Utokaji wa maziwa umepungua hivyo atakuwa anatumia nguvu kunyonya na hayatoki .

 • Kuota kwa meno kunamsababishia mtoto kukataa kunyonya ,sababu fizi zinakuwa zinamvimba .

 • Mama unapokula vyakula kama kabichi,maharage,jibini(cheese),broccoli, au maziwa ya unga (NIDO) inamsababishia kumpa gesi tumboni na anaweza kataa kunyonya haswa kwa watoto wachanga miezi 0-6 hapo.

 

Mama ni muhimu  kumnyonyesha mtoto  ,acha kutumia maziwa ya kopo kama unauwezo wa kunyonyesha , kama wewe unafanya kazi basi pump(kamua)maziwa mwachie house gal atampa mtoto ,yahifadhi hayo maziwa kwenye friji!

Kwa watoto wanaopewa maziwa ya kopo(baby formula)iwapo ameyakataa inabidi umbadilishie .

Please follow and like us:
error0

About afyaborakwamtoto

Hii ni Blog maalumu inayotoa elimu juu ya mambo ya uzazi na malezi bora kwa mtoto.

View all posts by afyaborakwamtoto →