Njia Za Kumwandaa Mtoto Kuwa Na Upeo Mkubwa(Akili)

Watoto ni wepesi kushika vitu na ni waelewe sana ,wanakuwa kulingana na malezi wanayopewa na wazazi. Wazazi wengi wanaamini mtoto huanza kufunzwa akiwa miaka 3-4 hapana tunakosea sana wenzetu nchi zilizo endelea wanaanza funza watoto wakiwa na miezi 6 hufunzwa kila vitu kulingana na umri mfano kusomewa vitabu mzazi unaweza ukaona haelewi hapana kichwa kinazoea kile anachofunzwa mara kwa mara  .

 image

Ukimwandalia mtoto msingi mzuri  tangu udogoni basi ana nafasi nzuri ya kuwa na upeo(akili) na  uwelewa mkubwa.Wazazi wengi wanaachia watoto wakiamini kila kitu watafunzwa shule ,hapana ni makosa mzazi inakubidi uchukue nafasi yako  pia  kuhakikisha unampa mwongozo bora mtoto .

Watoto wengine ni wazito kuelewa ️au kushika vitu kwa haraka hivyo vizuri akanza kufunzwa mapema.Maandalizi mazuri kwa mtoto yatamjenga kiakili na kumfanya kuwa bright. Hakuna mtoto mjinga duniani ni wazazi tu kukosea kuto kuwapa misingi bora watoto tangu wakiwa na umri mdogo.

 

 

Unatakiwa mzazi umsupport mtoto

Mtengee mda ujue ratiba yake akitoka shule anatakiwa kufanya nini,atacheza na wenzake kupumzisha kichwa kumbuka michezo ni muhimu kiafya,baada ya michezo afanye kazi za shule kwa kumsaidia,muulize leo shule wamefanya nini ?kipi kilimfurahisha? nini kilimkasirisha? ,masomo yalikuwaje itakusaidia kujua maendeleo yake ya shule na mahusiano yake na walimu na wanafunzi wenzake ,na unaweza mwelekeza homework yake.

image

 

 Wale wadogo wasio enda shule miezi 9-mpaka miaka 3 nao vile vile anatakiwa tengewa mda Wake ,anavyozidi kukua anazoea ile ratiba na kukaa kichwani kwamba nitacheza ila kunamda nitakaa kusoma hata kama dakika 10-20.

 

 

Njia za kuwakuza akili zao kupitia

 • Hadidhi-

  kuwasomea watoto hadidhi kunawasaidia kunajifunza maneno mengi mapya ,kuongea kwa haraka,inawajenga kuwa na kumbukumbu nzuri na wepesi wa kuchambua na kuelewa mambo kwa urahisi!

 

 • Vitabu na michoro

  Vitabu vya kuhesabu namba kwa kutumia michoro ya vitu,vitabu vya kuonyesha aina ya matunda na majina yake,vitabu ya kumfunza vyakula vitokanavyo na wanyama na mimea,vitabu vitakavyo mfunza maumbo kama duara,triangle n.k,vitabu vionyeshavyo vitu  asilia(mito,milima,mabonde,misitu n.k),majengo,usafiri na kujifunza kupaka rangi kwenye michoro ya vitabu itamsaidia kujua aina za rangi na wapi zinastahili kutumika kwenye michoro.

 •  image

 • Toys za kuchezea

  Toys za watoto zipo za kila maumbo ambazo anaweza jenga kama,reli,madaraja au  Lego(zipo za kila umri kuanzia miaka 2 na kueundelea ukienda Mlimani city utapata ),

 

 

image
KUJENGA LEGO UKIONA NI MCHEZO WA KAWAIDA ILA NI MZURI KUKUZA AKILI YA MTOTO
 •  Toys za wanyama anajifunza aina za wanyama  wafugwao nyumbani na waishio porini na wanyama wakali zaidi duniani,kujifunza vitu vya nyumbani kama vya jikoni n.k, Mfunze kujaza puzzle za namba au wanyama ,kucheza piano au gitaa

 

 

Michezo

 • Mfunze kuogelea ,kucheza mpira,kuendesha baiskeli,kucheza game za watoto una download kwenye simu yako au kama ana ipad za watoto nayo nzuri ila anacheza kwa kuzingatia mda kama masaa 2-3 kwa siku basi.Fatilia kujua hobby yake ni nini haswa .

Please follow and like us:
error0

About afyaborakwamtoto

Hii ni Blog maalumu inayotoa elimu juu ya mambo ya uzazi na malezi bora kwa mtoto.

View all posts by afyaborakwamtoto →